Wednesday, July 24, 2013

Word


Shalom
Kwa wale wote wanaotegemea kujifungua, mwamini Bwana Yesu kuwa atakuvusha salama. Usikubali shetani akujaze hofu hadi ushindwe kuifurahia safari yako ya ujauzito. Mkabidhi Mungu kila hatua na mtumaini kuwa anakwenda kufanya. Mistari hii uikiri na kuitafakari kila siku, itakuondolea hofu na kukupa tumaini.

FLP. 4:6-7 
"Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu."

1 PET. 5:7 
"huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu."

ISA. 26:3-4 
"Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. Mtumainini BWANA siku zote Maana BWANA YEHOVA ni mwamba wa milele."

ISA. 66:9 
"Je! Mimi nilete wana karibu na kuzaliwa, nisizalishe? Asema BWANA; mimi nizalishaye, je! Nilifunge tumbo? Asema Mungu wako."

Source:Woman of Christ

Reactions: