Monday, April 15, 2013

Wanawake wanajiuliza..

Kuna wanawake wa aina mbili duniani katika mapenzi kuna wanawake ambao wao wanayapenda sana mapenzi katika sita kwa sita hawaoni shida kufanya lolote ilimradi wawape wapendwa wao raha na huwa wanapenda kujifunza mengi kila wakati ili kufahamu mengi ya kitandani.

Na kuna wanawake ambao hawaoni faida kwanini wajifunze kwanini wao tu ndio waumize kichwa katika kujifunza ya chumbani kwanini wanaume na wao wasiumize vichwa ili wawaridhishe wanawake hawa huamini ukimwaga ugali wanamwaga mboga.

Leo nataka niongelee swala la mwanamke na ninagusia haswa waliokwenye ndoa ama wenye wachumba ambao wanatarajia kuingia kwenye ndoa, wewe mwanamke ni msaidizi wa mume wako MUNGU alikutoa katika ubavu wa mumeo upate kumsaidia ni jukumu lako wewe kumsaidia mumeo, wanawake tumepewa akili za ziada katika kujifunza na kuttatua mambo kiundani zaidi

Wanaume wengi hufundishwa mapenzi na wanawake wanaume wanatakiwa kupewa muongozo na mwanamke nd andio maana baba ni kichwa lakini mama ni shingo kichwa hakiwezi kuwa juu bila shingo kwahiyo mwanamke usiwe mvivu katika kujifunza mengi ya ndoa yako haswa chumbani kwasababu kama kufua hata baba anaweza kufua, kupika na yeye anaweza lakini kwakufundishwa na mwanamke kama sio mke basi alifundishwa na mama.

Lakini maswala ya chumbani ni wewe mke ndiye mwenye mamlaka ya kumfundisha mumeo hata ikitokea bahati mbaya ametoka nye asije akashangaa maana kuna wanawake wavivu kwenye sita kwa sita baba katoka nje kaenda kukutana na mtoto aliyefundwa mara baba kanogewa unaanza kulalamika na kupata mawazo mwanaume harudi nyumbani mara kabadilika kumbe mabadiliko hayo umeyasababisha mwenyewe ni bora ufundwe ujifunze ukampa hata akitoka akuikutana na aliyefundwa ataona hamna jipya na akikutana na ambaye hajafundwa ataona anapoteza tu muda na nguvu hakinogi bora cha mkewe..

Wanawake tafakari acha kujibweteka hizo zilikuwa enzi za zamani, watu sasa hivi wanajuwa maujuzi na maraha tele..

0 comments:

Post a Comment