Monday, February 25, 2013

WEWE...

Jamani natumaini hamjambo na weekend yenu ilikuwa muruwa kabisa, leo nataka kuongelea swala moja ambalo limemsababisha mtu wa karibu sana ninayemjuwa kuachika katika ndoa yake ikiwa ina mwaka tu na mtoto mdogo wa miezi miwili.

Wanaume tabia yenu ya kujifanya nyie ndio mnamapenzi sana na mama zenu inahusu!!! ndio tunajuwa kila mtu anampenda mama yake na ungefanya lolote usione mama yako anaumia lakini inahusu nini ukamuacha mkeo kisa kagombana na mama yako!!!! kama unampenda sana mama yako kuliko mkeo kilichokufanya uoe ni nini? inahusu???

Jamani heshima kitu cha bure mwanamke unapoolewa nenda kaheshimu kila mtu ukweni tena ukawapende huku ukitambua kuna chokochoko huko na zitakapokuja ujuwe jinsi gani ya kuzitatua bila kuleta balaa na kukosea watu heshima.

Kuna mama wakwe wengine jamani wanakero kisa mwanao kanioa nipo kwake ndio na wewe unataka kunitawala inahusu!!! kila unapoonyeshwa mapenzi na mke wa mwanao wewe huridhiki unataka unalolitaka wewe ndio lifanyike kwani wewe ndio mama mwenye nyumba ukibishiwa unakuja kuchonganisha maneno na mwanao.

Wanaume sio kila kitu unachoambiwa na mama yako unalibeba tu unafura kama kibuyu unaenda kugombana na mkeo na kutukanana kama unaletewa malalamiko siuwachukuwe wote ukae nao chini uwaulize matatizo ili mpate jawabu, wewe unajiona ndio una mama peke yako huyo mkeo sijui ulimchuma mtini ama wewe ndio unamoyo huyo mkeo ana jiwe haumii..badilika bwana

Tena mimi ndio nawatakaga hao wenye midomo iwe mama mkwe au wifi kutaka kujifanya kumjuwa sana mume wangu kisa ndugu yako inahusu, tena ukinipanda kichwani na chumba nakuachia tuone kama unaweza kumpa vitu ninavyompa mimi. Tujifunze keheshimiana wote tunampenda huyo mwanaume na wote huyo mwanaume anatuhitaji.

Reactions:

1 comments:

  1. Nilishawahi kumsusia wifi kitanda akalale na kakaake maana nilichoka.. Inahusu! Mwisho tukaheshimiana.. Yeye akafanya yake kama dada nami nikafanya yangu kama mke... Heshima mtu hupewa akijiheshimu na kuheshimu wenzake, asiyejiheshimu haheshimiwi.. Angalia monster in law movie utanielewa...!

    ReplyDelete