Sunday, January 6, 2013

Uswahilini kwetu....

Jamani wanaume tabia zenu hizo za kuona sketi barabarani ukashikwa midadi na kutaka kuifunua siku utakuja kuumbuka vibaya siku hizi wanawake wanajijuwa na wasiojijuwa wanapuliza kwa babu mwenziyo yule akishaenda pale anakupika unapikia anapewa na mikoba mengine ya kuja nayo kwako inakaa kwenye pochi.

Majuzi nilishuhudia mwanamke akiumbuka sehemu sema kwakuwa sikuwa nimebeba camera yangu nikashindwa kumpiga picha mume wa mtu baba wa maana anahela zake za haja katika pita pita zake akakutana na mdada wa uswahilini akampenda na kumtongoza wasichana bwana wanajuwa kunusa hela mwanamke akanusa akajuwa jamaa anazo hela zake siakamkubalia kukutana mara mbili jamanaa anahonga za haja mwanamke yule kazi yake msusi tu ana saluni yake sindio kuamua kwenda kumfunga sawa baba amalizie shida zake kwa babu bagamoyo.

Baba na kwambia ndio mapenzi motomoto tena kwa msichana wa uswahilini uswahilini ndio hatuhemi kwa mashauzi yake alikuwa anakaa chumba kimoja akaamia chumba na sebule mtoto akawekewa kila kitu ndani saluni ikafanywa ya kisasa mwanamke kanenepa kaanza na kujichubua ukimuona utamjuwa kama ndio alikuwa yule fulani tunapeleka watoto wakasuke kwake.

Yani kwakweli alipendeza kila mwanamke alimtamani, mwanamke akawa sio wa kupanda daladala tena akapewa dereva tax rasmi wa kumpeleka anapotaka bill mzee analipa mwisho wa wiki, na siunajuwa tena mtoto wa uswazi akipata anavyojuwa kuzitumia, siku moja alijiloga kwenda kukutana na yule baba na shoga yake wakaenda kiwanja gani sijui mikocheni huko wamelewa katika ulevi yule baba sijui alimshika kiuno yule shoga yake shoga naye kajibu basi shoga akichekeshwa anamlalia jamaa mara yule mwenye bwana sindio kukasirika na kuanza kupigana madongo ya chini chini basi maneno yakawa maneno mara wakaanza kutukanana sasa kwasauti kubwa sindio shoga mtu kumropokea mwenye mume kwamba asiyejuwa wewe unatumia hirizi nani kumkamata mwanaume mimi kanipenda sio kwa hirizi wala mzizi sindio mwenye mwanaume kukasirika na kuanza kubondana bondana ndio watu kujaa vipi?????

Ndio shoga mtu kuanzisha maneno mpaka ya uchawi kama hamuamini angalieni kwenye pochi, ndio pochi ya bidada tena kufunguliwa kukutwa na hirizi nyeusi tatu ndio kuumbuka mwanaume tena pale kupata kiwewe na kuwaacha na kuondoka, ugomvi ndio kuletwa uswahilini mwenye mwanaume kwenda kumfanyia shoga yake vurugu na kigoma basi vurugu mpaka kupelekana polisi na kulala huko wenyewe wanasema bado hilo alijaisha mpaka watoane roho..


Reactions:

0 comments:

Post a Comment