Monday, December 31, 2012

SHUKRANI ZA 2012.....

1: Napenda nikushukuru wewe ambaye ukiingia ofisini asubuhi na mapema kabla hujaanza kufanya reports na majukumu yako ya kazi unafungua libeneke na kusuuzwa moro halafu unapata nguvu ya kuendelea na shughuli zako...Ahsante sana


2: Nakushukuru wewe ambaye unajuwa kabisa kwamba hili libeneke nilakitanzania halafu upo nje ya nchi unapojisikia kutuma au kupiga simu kuuliza jambo huangalii muda wa kupiga tanzania ni saa ngapi unajikuta unapiga hata saa kumi usiku na kuniletea balaa kwenye ndoa yangu..Ahsante sana


3: Nakushukuru wewe ambaye unajuwa kabisa mimi ni mke wa mtu na profile yangu inasema hivyo halafu unanipigia simu ya kunitongoza na kusema imeandikwa kwenye libeneke kwamba natafuta mchumba..Ahsante sana


4: Nakushukuru wewe unayeniandikia email kuniambia mambo chungu mbovu kuhusu mume wangu na anayofanya mtaani unapomuonaga ukae kujuwa yule ni kidume na ukitaka hata wewe atakupa ni makubaliano tu, na email zako hazinifanyi nimuache na hatutaachana na ujuwe ubavu wa kuniacha yeye hana mpaka nitake mimi mwenyewe..Ahsante sana


5: Nikushukuru wewe mume wa mtu ambaye ukitaka kutongoza mwanamke unaanza kusingizia kwamba nyumbani kwako kuna matatizo na mkeo hakupi kabisa unyumba na mambo kibao kumbe ni uongo mtupu..Ahsante sana


6: Niwashukuru mahawara wote ambao unapotongozwa na mume wa mtu unajitapa kabisa kwamba kaona mkewe hafai ndio maana kaja kwangu mwenyewe unajidanganya nakutoa machejo yote ukiwa na moyo utazidi kupendwa cha kushangaza mume wa mtu mwenyewe hana habari ya kumuacha mkewe unatumiwa na kuachwa..Ahsante sana


7: Niwashukuru wanawake wote wanaoenda kuloga wapate ndoa wakiwa hawajiamini kwamba wao ni wazuri na wanastahili kupendwa na kuolewa, unaloga halafu unapata mwanaume ambaye hata dalili za kukuoa anakuwa hana unarudi kwa babu umekasirika dawa hazifanyi kazi...Ahsante sana


8: Nakushukuru wewe ambaye umri umeenda, umeolewa una watoto na bado unatafuta serengeti boy wa kukupa mzunguko, kama unajijuwa wewe umeenda umri na mabwana zako ni umri chini ya umri wako hiyo ni yako nasema..Ahsante sana


9: Niwashukuru wanawake wote wanaoolewa kwasababu ya kutoa nuksi ndio maana ndoa siku hizi hazidumu watu hawavumiliani wala hawabebeani misalaba wakiudhiana kidogo wanaachana..Ahsante sana


10: Niwashukuru wame za watu wote wakitoka majumbani mwao wamevaa pete zao za ndoa halafu wakiingia mitaani zinavuliwa na kuachwa kwenye magari..Ahsante sana


11: Niwashukuru wame za watu wote ambao wakipata hawara mpaya usiku huo wanalala hukohuko mpaka asubuhi na wakirudi nyumbani wanasingizi walipata matatizo..Ahsante sana


12: Nawashukuru wame za watu malaya wote ambao wanapogundua au kuhisi wake zao wanaliwa nje wanawapiga na kuwafukuza nyumbani wakati wao wenyewe ni malaya mbwa kweli mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu..Ahsante sana


13: Niwashukuru wanandoa wote wanaotoka nje ya ndoa zao nakufika kwa mahawara zao wanajipinda na kutoa machejo ya mzunguko ambayo ndani ya ndoa hamna kabisa..Ahsante sana


14: Niwashukuru mahawara wote ambao wakikutana na wame za watu wanalia na kumsifia mwanaume kwa raha anazopata wakati mioyoni mwao wanajuwa wanaumizwa hakuna raha yoyote bali wanamuibia baba wa watu ukitoka hapo unamsifia sana kwakuwa unajuwa unaachiwa pesa nyingi wakati moyoni unamtukana..Ahsante sana


15: Nikushukuru wewe mume wa mtu unayewekwa mjini na mkeo lakini kutwa barabarani huishi mahawara wakati hata hizo hela za kulipia gesti umeachiwa na mkeo asubuhi za mishemishe mjini..Ahsante sana


16: Niwashukuru mahawara wote ambao wanajuwa wanatongozwa na mwanaume ambaye hela hana halafu wao wanachukuwa jukumu la kutoa hela zao na kulipia gest akapewe mzunguko..Ahsante sana


17: Niwashukuru wame za watu wote ambao wanaondoka nyumbani hela za matumizi hawaachi wakisema hawana hawajapata halafu jioni unampigia hawara unampa mzunguko na kumuachia hela ya matumizi..Ahsante sana


18: Niwashukuru wame za watu wote wanaopenda wanawake wazuri hapa mjini na kuwasifia uzuri wako na kuwatamani wakati wewe mkeo hata hela ya kujipamba humuachii nyumbani anachakaa kwa kulea nyumba na watoto..Ahsante sana


19: niwashukuru wake za watu wote ambao kisa kaolewa hataki hata mama mkwe aliyemtunzia huyo mumewe aje nyumbani kusalimia akisema kaolewa na mmoja sio na ukoo mzima..Ahsante sana


20: Niwashukuru watoto wote walio chini ya umri wa miaka mitano ambao kutwa wanalilia kulala chumbani kwa wazazi halafu ikifika saa saba baba akitaka mzunguko mtoto anaamka na kuomba maji na kumkuta baba juu ya kiuno cha mama na kuanza kulia anamuumiza mama halafu mzunguko unaisha katikati kabla ya kufika kileleni..Ahsante sana


MUNGU akipenda tukutane tena 2013....GraciasReactions:

2 comments:

  1. Hahahaaaaa nimechekaje?

    ReplyDelete
  2. Ha ha ha ha ha nimependa namba 4,5 na 6, well said dada, ha ha ha ha ha

    ReplyDelete