Friday, December 21, 2012

Laana...

Wapendwa leo nataka niongee na wame zetu kama unajuwa wewe ni mume wa mtu hii inakuhusu, mume tambua kitu kimoja tokea ulipozaliwa ulikuwa unaweza kupata laana moja tu ni kutoka kwa mama yako mzazi ndiye aliyeweza kukulaani ulipokosea na akikunya moyo wake najuwa mnajuwa kwamba hakuna tena mafanikio hapo.

Baada ya kuoa laana nyengine ikaongezeka katika maisha yako ni laana ya mke wako najuwa wengi haya yamewakuta labda ni kwavile hatuwi wawazi katika mambo hayo lakini hakuna laana nyengine mbaya kama laana ya mke.

Wengi tumewaona kwenye jamii baada ya kuoa wakafanikiwa sana lakini katikati ya ndoa zao wakawadharau na kuwanyanyasa wake zao labda hata kuwafukuza na kuoa wengine na baada ya siku kadhaa wakaporomoka sana kimaendeleo wengine wakajikuta baada ya kuachana na wake zao wakaanza kuwa na wanawake tofauti nje wakajikuta wanapata magonjwa na wengi kupoteza maisha.

Tunapenda sana kuwachukulia wake zetu poapoa kabla hujamuoa mapenzi yalikuwa motomoto outings haziishi, mazawadi hayaishi na maneno ya mahaba ndio kila dakika lakini baada ya kumuoa hakunaga tena kitu kama hiko hapa nikiuliza lini mara ya mwisho ulimwambia unampenda mkeo wala hujui, nikuuliza hata kama unakumbuka siku yake ya kuzaliwa ndio hujui kabisa, na je lini hata ulimchukuwa mkeo na kumpeleka hata bar ya jirani ukamnunulia soda moja kama sio mnywaji wa beer ndio kabisa wewe kutwa na marafiki kwenye mabar mnyweee na mtafute na wanawake cha muhimu kwako unajuwa nikifika nyumbani nikitaka mzunguko yule mama atanipa na chamuhimu ninahela ya kumuachia kesho asubuhi hiko sindio cha muhimu kwake.

Kutwa mkeo alee watoto wenu, aende na yeye kutafuta riziki, arudi nyumbani wasichana wa kazi wamsumbue kichwa na kuzozana nao kuhusu kuweka nyumba sawa na kama hamna wasichana wa kazi akirudi aanze kufanya usafi na kuweka nyumba sawa, akupikie pamoja watoto halafu wewe unarudi saa tisa usiku aamke akufungulie mlango huo usiku akutengee na akae na wewe ule chakula na labda huli uende ukalale na labda usitake kulala ukataka akupe mzunguko hata humuandai vizuri ilimradi tu umemaliza shida zako kweli hii ni ndoa unategemea mkeo anapoamka asubuhi akiwa anasali atakuombea kwa mapenzi mema????? hapana  kuna kipindi mimi rafiki yangu aliniambia yani Rose siku nikiwa mjane nitafurahi sana kuliko kuishi maisha haya unajuwa unamume kumbe sio chochote wala lolote mateso tu.

Wazazi wenu wapo mjini au ndugu zenu mnao waamnini hata siku moja umeshawahi kumwambia mkeo tupeleke watoto huko kwa siku mbili tu ukamchukuwa mkeo mkaondoka hata hotel ya mjini tu au bagamoyo mkaenda mkiwa wawili tu mkaonyeshana jinsi gani bado mnapedana na mnamapenzi bado yanachemka kama zamani ni kazi na kulea tu ndipo kunawafanya msipate muda wa kukaa pamoja, mkitumia siku mbili kila baada ya miezi mitatu kuwa pamoja na kwambia huyo mama hata siku ukimkosea atajuwa ni shetani ama bahati mbaya maana bado unampenda na kumjali.

Hukujuwa hilo baba chukuwa ulitendee kazi huyo mama siku zote atakuombea na utafanikiwa sana kwakupitia maombi yake.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment