Friday, December 21, 2012

Jitambue....

Jamani wanawake na wanaume kuna mambo mawili leo nataka niongelee kuhusu kufumania wame/wake  zetu, kwanza kabisa mwanzo wa dunia wakati MUNGU alipomuumba adamu na hawa akawaweka katika bustani na kuwaamuru wale kila tunda kasoro la ule mti wa laana lakini sote tunajuwa ilivyotokea baadaye nini akaja shetani akamponza hawa mpaka akala lile tunda na siyo yeye tu hawa akafanikiwa kumshawishi adamu na yeye akala tuna na wakajikuta wote wamemkosea muumba wao ndio maana mpaka leo tupo hapa tulipo.

Kwanini nimewapa huo mfano nataka muelewe jambo ambalo linasumbua ndoa nyingi sana na kwasababu wanandoa wengi hawajalitambua ndio maana ndoa nyingi sana zinamatatizo na nyingi sana zinavunjika na nyingi sana hazina amani wanaishi kulea watoto tu na wengine hawalali pamoja wametengana vitanda, vyumba au hata kama wanalala pamoja basi ni mzungu wa nne.

Ukiwa kama mwanamke au ukazaa mtoto wa kike utambue jambo moja ya kwamba wewe unaweza ukawa katika mpango wa shetani mpango gani tokea siku ya kwanza wanaume wamekuwa ni wadhaifu sana kwa wanawake yani hata kama mwanaume ni hodari kiasi gani lakini hana nguvu za kupindua mipango ya mwanamke wamekuwa wadhaifu sana kwa wanawake.

Wewe kama mwanamke unapotongozwa na mwanaume ambaye kabisa unajuwa ni mume wa mtu mwenyewe unajisifia kabisa mkewe atakuwa hamtunzi vizuri ndio maana kanifwata miye tena unajisifu kabisa chezea miye..rubbish kabisa unajitapa bila kugundua shetani amekutumia wewe kumuharibu huyo baba kumtoa katika mpango wa MUNGU unaosema alichokiunganisha yeye hakuna wakukipangua kwahiyo kabla hujamkubalia huyo mume wa mtu ujuwe kama na wewe upo kwenye mpango wa shetani.

Au wewe mke wa mtu unapotongozwa pia nakutamaniwa na wanaume na wewe pia unakuwa katika mpango wa shetani kwakuwa huo sio ubavu wako ubavu wako ni mumeo lakini siku hizi tunajidanganya kwani inaandikwa usoni kama ninauhusiano na mumewe au mkewe haijiandiki leo lakini siku tukiwa katikahukumu ya aliyejuu ndio utaona itakavyojiandika na utakavyoumbuka.

kwahiyo mwanamke unapojitapa kuwa na huyo mume wa mtu au wewe mwanaume unapojitapa kuwa na huyo mke wa mtu kumbuka umeangukia katika mpango wa shetani wa kuharibu ndoa za watu na sio uzuri wako au hela zako zimekufanya umpate bali umempata kwa masaada wa shetani..jitambue sasa na ufanye maamuzi mema kila unapoishi katika dunia hii.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment