Tuesday, November 6, 2012

Nimeikuta hii sehemu..

ACHENI NIWAPE HESHIMA WANAWAKE WOTE DUNIANI KWA YANAYOWAKUTA:

 
Imagine:

 
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza, anakuelewa, anakusamehe - halafu anasahau.

 
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anachukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!

 
UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI: Anakukaribisha, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.


UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake) Unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!

 
CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hamna maandalizi unamuumiza. Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza kutokea. Hana kinyongo!

 
UNAJIANDAAA KWENDA KIBARUANI: Unakuta kashakuandalia viwalo, suruali imenyooshwa kama ya askari trafik, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi! Ulichomuudhi jana kashasahau na kukusamehe!

 
UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuchia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!

 
Na mengine meeeenggggiiiiii sana wanafanyiwa hawa watu lakiniWANASAMEHE, WANAVUMILIA! Ni watu muhimu sana hawa watu maishani mwetu!HIVI INGEKUWA WANAUME WANAFANYIWA HIVI INGEKUWAJE?

Reactions:

0 comments:

Post a Comment