Friday, November 9, 2012

Msaada tutani..

Dada Rose

Mimi ni mwanaume nimeoa mwaka wa tatu sasa ninatatizo kubwa sana katika ndoa yangu, mke wangu anakataa kuzaa kabisa sio kwamba mimba hapati ameshapata mbili na ametoa zote anasema kwamba hataki kuzaa harakaharaka anataka kwanza ale raha za ndoa ndio azae. Mimi nataka mtoto tumeshakaa miaka mitatu sasa na yeye bado tu hajatosheka na hizo raha za ndoa kwakuwa mimba anazibeba yeye nakosa la kufanya naombeni jamanai mnishauri huyu mwanamke nimueleze nini ili anielewe??? anasema bora hata miaka mitano ipite ndio azae kweli kuna mtu anaweza kuvumilia miaka mitano yote bila watoto ama analake jambo na mimi maana simuelewi kabisa.


Julius

Reactions:

3 comments:

  1. uyo mkeo c bure jrb kumchungaza vzr,mna hkn mtu asiyependwa kuitwa mama ktk dunia hii espacial waafrica.

    ReplyDelete
  2. Rose natafuta mwanaume wa kuzaa nae hebu aje nimzalie mtt mie

    ReplyDelete
  3. Hizo mimba anazotoa siku akijakuhitaji huyo mtoto asipopata itakuwaje? embu muulize kwanza. Maana anakuwa kama hana akili timamu. Aache ujinga azae watoto. Anataka raha akale kwao hizo raha.

    ReplyDelete