Tuesday, October 2, 2012

SOMO...

Somo langu la leo liwaendee wanawake wote wajawazito uwe ndani ya ndoa ama nje ya ndoa, hivi mwanamke inahusu nini kisa mjamzito kumnyima mumeo unyumba????? ulivyokuwa unaitafuta hiyo mimba mbona ulikuwa unampa mara kwa mara hata kama akikwambia kachoka wewe unataka basi amani hamna hapo ilimradi tu upate, sasa leo umepata ukiombwa wewe hutaki unasema mimba inakufanya ujisikie vibaya mpaka umsumbuwe kaka wa watu wee ndio unaona raha au unadhani pakumalizia shida zake unayo wewe tu kila mwanamke unayemuona barabarani anayo shoga kukuweka ndani na kuitaka yako muda wote ni jambo la heshima sasa kwanini ujishushie heshima yako kwa yeye kutaka nje kisa wewe unamnyima..allaaaah haiendi hivyo tena ni aibi kubwa sana mwanaume kutoka nje ya ndoa kisa wewe unamnyima unyumb..hukufundwa wewe..

Tena wanawake wengine wakiwa wajawazito akishamuona mumewe kaja ndio mdomo atauvuta umepida kama kisu cha kuparuria ndizi inahusu, kisa cha kumtesa mtoto wa mwanamke mwenzio ni nini???? kwani yeye kwa kukuoa wewe alikuwa anataka kufuliwa maana madobi wapo tele, kama alitaka chakula shoga hata kwa mama ntilie angeshiba, mwanaume anataka kutunzwa anataka apewe mambo kwani huko barabarani kaona wanawake wangapi mpaka akuweke wewe ndani na umzalie watoto au unaona kizazi unacho weye tu jamani wanawake haipendezi..

Wewe baba uliyenitumia hii endelea kumbembeleza mkeo, labda kwa upande mwengine unajuwa kuna mimba nyengine bwana zinavituko kama zilikuwa zimetungwa watu wakichuchumaaa yani mimba utakuta inamchukua baba mwenye nyumba mpaka kero, yani wewe heri ulale nje kuliko kurudi nyumbani yani mkeo akikuona anataka kufa, kwahiyo usichukulie tu mambo kirahisi maana simpaka mmempima mkakuta hana tatizo zaidi ya mimba basi labda kati ya zile mimba zinazomchukia baba na hiyo moja wapo. lakini kutoka nje ya ndoa sio tatizo endelea tu kwa mapenzi tele kumuomba mkeo atakupa tu ila mvumilie sana..

Siku yetu ya kufundwa tarehe 21/10/2012 pia tutafundwa jinsi ya kuchuma tunda ukiwa mjamzito ningekushauri mkeo aje pia ili akiona pale aweze kujifunza na kukupa raha unayostahili..

Jamani hii ni kufundishana mambo yaliyopo mwanamke ndoa bwana mwanamke nyumba sio kuta tuu zimesimama na wewe ukajiita mama mwenye nyumba...hehe heiya unaujuwa umama mwenye nyumba wewe kama hukujuwa njoo tukujuze shosti...

Reactions:

8 comments:

 1. Habari, nimepata tatizo kidogo na hii post yako,nadhani ungetafuta ushauri kidogo tu kutoka kwa wataalam katika hili.
  Mtu anapopata mimba kuna mabadiliko katika level za hormones,hizi ndizo zinasababisha tabia fulani fulani. Labda yeye tendo la ndoa kwa wakati huu ni tatizo kwake. Kila mtu anareact tofauti, hata aliyekuletea mada amesema wamepima wamekuta tatizo ni mimba, sasa yeye na wewe msichoelewa ni nini?
  Tatizo hapa sio kutofundwa,huyo mwanaume anatakiwa kuwa muelewa wote wanataka mtoto otherwise asingempa mpa hiyo mimba. Huyo dada anahitaji faraja sio kusimangwa....! Mi sijazaa bado, nilidhani mliopitia hayo mtakuwa waelewa ila naona ni tofauti. Sijapenda the wording, huo ni mtazamo binafsi

  ReplyDelete
 2. Jamani naomba tuelewane kwenye hili huyu baba analalamika mkewe kwanzia kapata hiyo mimba mpaka sasa hataki kumpa tendo la ndoa..kweli jamani sijui wataalamu inawezekana miezi saba nzima hizo hormones zinampelekesha mtu asifanye tendo la ndoa kweli????? mimi nimezaa mara mbili ndio inatokea wakati mwengine hujisikii kabisa kufanya tendo la ndoa lakini sio zaidi ya mwezi ni mara chache yani hata kwa mwezi unashindwa kumpa mwenzio mara tatu tu mmhhhh..nimekataaa hizo hormones sasa zitaleta matatizo kwenye ndoa za watu... huo ni mtazamo wangu..

  ReplyDelete
 3. Binadamu tunatofauti nyingi ikiwemo hiyo ya tabia wakati wa mimba. Kuna ambao hawasikii chochote japokuwa na wao hormones zinakuwa zimebadilika, kuna wanaokuwa wagonjwa from the day they conceive mpaka wanajifungua na tabia nyingine tofauti kulingana na mtu.
  Watu wanaokuwa wagonjwa from the beggining wapo, wazima through out wapo, wanao kuwa na mabadiliko kwa kipindi kifupi pia wapo. Bado sikubaliani na wewe, kama inakuwa kwa muda mfupi kwa majority, wapo wengine wachache inaweza isiwe hivyo. Nina mfano halisi wa mtu aliyekuwa mgonjwa muda mwingi, ndio maana sikubaliani na wewe, alafu wameenda hospital wakaambia ni mimba, what else do we need to understand? Labda kama hilo tatizo ni spiritual, otherwise I still dont agree

  ReplyDelete
 4. Itakuwa ngumu aisee...mwanzo wa mimba mpaka mwisho......sipati picha hata siku moja tu kumpa mzee..hahahahaha ukiambiwa kua uyaone sio maghorofa ya posta mambo ndio hayo..ila bado nakataa tutaendelea kubishana kila mtu na mtazamo wake ila nyie wenye mimba mjitahidi sana aisee kama mnapenda ndoa zenu kila kitu kinaanzia kichwani ukishafikiria nataka kufanya hiki utafanya tu no matter how your hormones zinakupeleka na zikikupeleka kukataa..Tupa huko kwenye dustbin what to do they are called hormones..haha

  ReplyDelete
 5. Nimesoma comments zote ila Da Rose zako nimezipenda, we ndio umenielewa, labda sababu umekuwa ukikutana na case mbali mbali za jinsi kama hii. Mimi ni yule kaka mwenye mke mjamzito, anayekataa kutoa mambo yetu ... kila siku amechoka. kuna mmoja amekoment amesema "Huyo kaka anatakiwa awe muelewa" pia amesema "mi sijazaa bado" muwe makini na vijana wengine wanarukia mambo ya kikubwa kabla ya umli,mi nadhani mambo ya ndoa yajadiliwe na walioko ktk ndoa,ingawa nao vijana wana mawazo mazuri ila wapewe limitation.Tangu mwenzangu
  apate ujauzito nimepunguza zile frequency za ku pata ..., badala ya mara 2 kwa wiki, sasa hivi naangalia hali yake,ninapofikia ukomo yaani hali mbaya naulizia leo vipi darling safi? unaambiwa
  mhhhhhh !!! sitaki kabisa, tena usiniguse anajibu,mpaka siku nikihitaji ujue hali ni mbaya nakuwa kama naumwa,natetemeka kwa hali hii nimeelewa kwa nini wanaume wengine wasioweza kujicontrol hubaka. juice,ndizi,ubuyu vyote anavyohitaji namnunulia,kwa tabia hii ya mke wangu nilikuwa namuona house girl mbaya tangu ameanza tabia hii namwona house girl anapendeza na vipita njia wote wazuri tangu nimeoa nilifunga mlango kwa msichana yeyote asiye mke wangu, ila nawasi wasi nisije uvumilivu ukanishinda ndio maana naomba ushauri sehemu mbali mbali, nina akili timamu siwezi kuchukua kila ushauri nitauchuja kwanza.Niliwahi kuona article furani sijui humu ktk blog yako Da Rose au wapi, ilikuwa inaelezea kuwa mwanaume akikosa mambo yetu ... kuna uwezekano wa kupata prostate cancer naogopa.Niendelee kuwa mwelewa tusubiri mpaka ajifungue au niendelee kujitosheleza pale manii zangu zinatoka zenyewe ninapoenda haja ndogo au kubwa.Mimi mpaka niliamua kuoa baada ya kuona uhitaji wa mambo yetu ... ni mkubwa, nikaona kwa nini nipate ukimwi wakati Mungu ametuumbia wasichana wengi wazuri unachagua unayemtaka, mweusi,mweupe, aliyejazia,tall, flat, anayejikoboa,natural etc.Asante kwa taarifa ya semina ya tar 21/10/2012 mamaa nadhani akijisikia vizuri nitajitahidi asikose, nitaendelea kuifuatilia blog yako Dada Rose nakushukuru tena kwa kuiweka mada hii mezani ili watu mbali mbali kwa kutumia hekima zao walizojaliwa na Mungu tujenge wala si kubomoa. NAKUTAKIA KAZI NJEMA

  ReplyDelete
 6. mi naungana na mchangiaji wa mwanzo kila mimba ina vimbwanga vyake!we rose hujapata complications kwenye mimba ndo mana unasema hivyo.mshukuru sana mungu kwa hilo.mi nadhani hiki nikipindi ambacho mume anatakiwa awe na uvumilivu mkubwa kwani akisubiri anakufa?huyo atabaki kuwa mkewe na baada ya mimba atampa mpaka achoke!we kama mimba haikukupa kisirani basi mshukuru sana mungu!ila wote wanatakiwa kuchukuliana na siyo kulalamika.

  ReplyDelete
 7. we kaka acha kujidanganya kansa?mhhhh!makubwa.naamini ingewezekana upewe hiyo hali ya mkeo hata kwa siku tatu tuu itakuwa balaaa.kwanza utamsifu mkeo kwa ujasiri alionao.mimba si maleria inayopotea kwa siku 2 kaka.na kama kweli hhuyo ni mkeo wa ndoa sioni tatizo la wewe kulalamaaa hivyo.kwanza mpaka ukae chini na upost hii habari humu tayari mtu kashajua wewe ni mwanaume wa aina gani.usije juta kwa tamaaa bure ya kushindwa kuvumilia.muache mwenzio kama hajiskiisafari ikiiisha mtarudi kw gemu kama kawa!usiendeleze mtandao wa ngono kwa tamaa zako!hukujua maana ya ndoa kabla ya kuowa thats why!

  ReplyDelete
 8. Majadiliano mazuri sana. Suala la "homoni" na hisia tofauti za kila mwanamke(anavyojisikia) ni muhimu kwel kwel.
  Ila kuna moja ambalo halikuangaliwa kirefu. Ukweli ngono wakati wa mimba husemekana pia nzuri (na muhimu) kwa mja mzito maana husaidia kufungua mfereji wa uzazi na uke (kipenyo cha nje na ndani)...hasa kama mwanamke hajawahi kujifungua au hakuzoea kulala na wanaume wengi ujanani. Hisia za ngono husaidia (na hii ni sayansi si maneno matupu ) kutanua mishipa na nyama nyama zote ndani ya kizazi... vile vile shahawa hulainisha na kusaidia kurutubisha ulingo wa mama mzazi. Tunavyojua shahawa ni proteni za hali ya juu sana. Vyote pamoja na mapenzi baina ya mke na mme huchangia kusaidia afya ya mtoto tumboni, hisia za mja mzito na maisha ya baadaye ya familia.
  Sisi tuliobahatika kuishi ughaibuni...hasa wanaume tumeelemishwa sana na utaratibu uliopo huku wa kuwalazimisha madume kuwepo wakati wa kuzaa. Inafungua macho ingawa haizoeleki.

  ReplyDelete