Friday, October 5, 2012

Msisitizo...

Wapendwa nasisitiza tena hii shughuli tunayoifanya kama wewe unahisi unajambo unataka liongelewe pale basi nitumie email ama message, narudia hii sio kitchen party ya kufundishwa maisha kwa mafumbo humu tunafundwa kwa uwazi na maneno yanatajwa kama yalivyo hakuna mafumbo wala aibu kwahiyo narudia kama wewe ni wa aibu jiandae na kama wewe ni mtoto usije sisi tunataka waliokomaa na wenye kuhimili mambo..

Hakutakuwa na picha wala video yanayofanywa humo yanaachwa humo.

Reactions:

1 comments:

  1. Wajawazito kutokula baadhi ya vyakula.
    Nakubali kabida Boss kuhusu imani na taboos ulizozisema kuhusu mayai huko uchagani na kwingineko. Hasa inakuwa hivyo kuzuia mtoto kuzaliwa mkubwa na Fistula zilikuwepo zamani pia-unasikia wanasema 'yule mama anayenuka mikojo'. Umasaini ndio kabisa mama mjamzito analindwa asile virojorojo kuogopa kuzaa mtoto mkubwa na mama kufariki. Ukiongeza female Genital Mutilation (Excision) au cliteridectomy wafanywiwayo baadhi ya makabila uliyoyataja hapa, inaleta tabu katika uzazi salama. Isipokuwa, wazee wanaelewa kuwa Kipara si issue hasa ni jinsi ya kumtisha tu. Lakini mtoto wa Mmasai for example anazaliwa njiti mpe miezi 3 ni mkubwa kulikoni kutokana na lishe bora ya maziwa, mtindi etc. tatizo ni TB tu kwa watoto wadogo pia kutokana na maziwa kutokuchemshwa wakati mwingine. Lakini mtoto wa Mchanga-Kwashakoo kubwa na waliongoza miaka ya nyuma sana katika child malnutrition and undernutrition. Anazaliwa kilo 3 mnene, likizo ya mama miezi 3 analishwa mtori na supu za maharage; likizo hiyo ikiisha mama ni punda zizini na migombani, gulioni kutwa na kupika mbege auze mapaka usiku mzee aje kujinyakulia fedha hizo kwa biashara DSM na mijini mama anadhoofika, mtoto analelewa na bibi kizee mama mkwe hali ya mtoto inakuwa mbaya.

    Mpare yupo kwenye mifongo kutwa kilo zake ukimpima BMI inaonyesha ana mtu mzima underweight lakini yu hai busy daily baba kuchunga mama kilimo cha kiangazi, masika, vuri na kulinda usiku mazao yasiliwe na wanyama pori. Chakula ni Msele (Fagara) easy to cook lakini haina lishe inateleza tu vema kooni; akichuma bwete na msele majani pori anayachemsha sana anamaliza vitamini na kamtindi juu ka kumezea ugali. Afya inaathirika, snack ni muwa. Ila ninawasifu wanaongoza kwa kula mazao pori natural medicine. Ni hivyo banana culture Bukoba na women's workload imeweka afya ya watoto vibaya-consult nutritional report. Hao wangazija hakieleweki na ndio maana coastal areas kuna resources nyingi-samaki, mboga pori, kisamvu kinalimika you name it lakini uvivu wa kujituma, mapishi ya kuchemsha sana kukamua na kuosha na kupika inaadhiri afya na lishe duni, magonjwa ya ngozi ya ukosefu wa madini muhimu-ukurutu mwekundu na mabaka yake prevalent. Bado kichocho kwa kuoga mabwawani na mitoni asilimia 80-100 kwa wanafunzi/watoto na mijitu mizima pia. Kula vitamutamu, samaki na yama ya kupaka nazi nzito kulinda ndoa na kula shatashata kupendeza macho ndio vinapelekea high BP, na paralysis (wanaita kiharusi). Nazi inaua na inawamaliza.Isipokuwa wanahusisha madafu na nazi na magonjwa ya matende sio BP lakini haswa ni mambu culez yanayozaana chooni na mabwawa ya maji machafu. Pamoja na climate change na kuongezeka joto na tulicyo wachafu ktk mazingira itafurahisha wangazija na wazaramo kuona wasukuma na wachaga wanapeta na matende na ule mwingine.

    Ukiwauliza wazee watakwambia hata pale waliposema 'Nyumba Ngitu' kwamba ukiukata mti ktk pori utakufa au Mungu atakasirika mvua haitanyesha. Ukichotea ndoo ya chuma maji yatageuka mekungu uchotee kata ya kibuyu; mama asisafishe Ndiwa (water reservoir ya umwagiliaji) maji yatakauka au kugeuka mekundu-ni kwamba walizuia deforestation kuzuia msitu wa Miungu usikatwe walijua huo ni tegemezi kama water source. Mbona wanakata sasa na kuchoma mkao, kupata mbao hawajafa. Isipokuwa mito inakauka, kilimo kinaathirika. Wale wa ndiwa walijua mwanamke akiingia humo nguo itapanda juu, kama yupo ktk siku mbaya maji yatapata rangi nyekundu. Ni fedheha kwa mama afunue nguo ndio asafishe bwawa la kumwagilia. Ukiacha kuchotea kibuyu utaharibu maji kwa ndoo ya chuma yenye kutu (maji kuwa mekundu Mzimu wa kisima umekasirika). Plastiki si zimekuja juzi tu? Indigenous knowledge ya hii miiko na maana zake kwa sasa tuichambue na tuitumie ile mizuri positively tukielewesha wahusika maana itakiwayo wasiichukulie vile ya mafunzo ya pseudo science. Zile potofu na uharibifu wa afya na haki za binadamu na mazingira etc tuziangamize hadi kwa kutumia sheria inapobidi Ndugu Chachage.

    ReplyDelete