Monday, September 3, 2012

Me and My gals at our friend's house in Kibamba...uuuiii nilijuwa naenda Morogoro safari ni ndefu


Prince naye alikuwepo, uuiii nampendaje huyu mtoto ni mzuri yaaanii..


Huwa namwambia mama yake inaelekea siku ya kutungwa Prince walikuwa na furaha na mapenzi tele maana amenogaje sasa..sura ya baba weupe wa mama...


Mama mwenye nyumba chezea kipenzi cha Jigge wewe. toto la Kichagga, shoga maana shurti kufungiwa kibamba nyumba moja hapa nyengine huko siye tuliozoea vigodoro huku patanishinda..


Wapi mama Prince mwanamke jicho, mwanamke rangi hakunaga carolite hapa za kutoana sura za chapati chunusi na makovu hayaishi inahusu!!! Chezea toto la Kichagga


Hahaha Mama PJ maana maneno tuliyokuwa tunafundwa siku ile lazima uwaze kama kwako yamo ama hayamo..mtoto hata ukiwaza unang'aa na kupendeza kweli hapana chezea toto ya Kichagga


Hapo sasa mama Prince alikuwa anaongelea Ubunifu wa mwanamke katika nyumba..jamani sitakaa nisahau


Wapi kipenzi cha Jigge na mwanaye Eddy


Hapo siye watoto wa Kilimanjaro express tukisikiliza kwa makini ufundwaji..Mrs Mizizi nikimsikiliza kwa makini Mrs Anorld akikazia mada kuhusu raha ya chumbani..Wapi mama Mbonde.. hehe heiya...


Usiku ukaingia kikundi bado kimepamba moto..


Na huko kibamba kulivyo na upepo na hivi nyumba za kuhesabu we acha tu tulitafutaje kanga..


Kufundwa kukiendeleaReactions:

0 comments:

Post a Comment