Tuesday, September 25, 2012

Lahaula..

Hivi leo nataka niongee na kina baba haswa na wanaume kwa ujumla wote wanaotegemea siku kuingia katika ndoa.

Hivi wewe mwanaume unapomuona mwanamke barabarani kapendeza ukamtamani na kutaka kumtongoza unafikiria nini? huo uzuri na mvuto wake unaokufanya uwashwewashwe kama umepandiwa na washawasha ni nini, kisa mtoto kapendeza, anamvuto sindio wewe huku roho juu kama povu la bia sindio??

Sasa inakuwaje wewe baada ya kumtongoza mtoto wa watu na yeye kakubali mara mkapanga kuoana ndani ya ndoa ukaacha kumuhudumia??? hii inahusu nini yani mimi sipendi kabisa tabia za wanaume wengine kama hivi huu ni ushenzi kabisa mwanaume mzima umuhudumii mkeo halafu kutwa jogoo linawika kutafuta wanawake wengine wa barabarani halafu unajisifia tatizo mke wangu hajiweki sopusopu..pumbavu kabisa

Yani mimi nakerekwa haswa, nina rafiki yangu mmoja jamani ni mdada mrembo sana, yani sana alikuwa anajipenda hakuna mfano hakuna style sijui ya mapochi wala nguo iingie asiwe nayo, mpaka kupendwa na kuolewa na mwanaume mzuri tu na mwenye pesa zake sasa yupo kwenye ndoa kama mwaka mwanaume haijui hela yake na mpaka matumizi ya nyumbani mwanaume anataka aandikiwe kwenye karatasi akanunu mwenyewe jamani hii inahusu nini sasa na mkewe kazi hana alimkataza kufanya anataka awe tu nyumbani alee watoto wao.

Kwani nyie kina baba hamjui katika zile hela za sokoni ndio kidogo mama akibana anapata hela ya kushonea weaving, hivi wewe unadhani mkeo kazi hana hela uumpi unategemea akatoe wapi mpaka pedi akuombe umnunulie hii ni sawa? hukufundwa wewe??? yani natamani hii siku yetu ya kufundwa na wababa nao wangekuwepo tuwape vidonge vyao sio sisi tunafundishwa kuwajali nyie halafu nyie mnafanya matapishi ambayo hata wewe mwenyewe unayoyatapika huwezi kuyafuta..inaniuma sana

Madada wa watu alivyomzuri yani ukimuona mpaka roho inakuuma mwanaume anamafari matatu lakini hataki mkewe aendeshe hata moja kweli mkeo ni wa kupanda daladala na wewe umepaki magari na hutaki aguse!!!!!!! halafu ukirudi nyumbani saa saba za usiku unamuamsha akupikie chakula eti wewe unakula chakula fresh kilichotoka jikoni hutaki cha kupashiwa halafu mkeo unamfanyia dharau!!!! yani natamani hata kutoa chozi nikikumbuka

Jamani wanaume mwanamke ni pambo, ukilinyausha atatokea wa kulipalilia na likang'aa wewe utatupwa huko, usione watu wamedumu na wapo kwenye ndoa ukajitapa mke wangu ananipenda, sijui najuwa kumtunza kumbe mwenzio yupo kwasababu ya watoto wako wewe ulishawekwa huko kwenye uvungu wa kitanda mwanaume mwenzio ndio anatawala mawazo na moyo wa mkeo!!! unapenda iwe hivyo???

Sote tunapenda na kuheshimu ndoa zetu ndio maana tumekubali kuoa na kuolewa na tulio nao, basi tujitahidi kuwatunza na kuwapendezesha sio unamkuta mwanamke mdogo lakini kazeeka kuliko mumewe mpaka mkienda kwenye shughuli mwanaume anakutanguliza mbele maana anaona aibu kutembea na wewe watu wasimcheke mwanamke sura imekukunja kama umelamba mbilimbi..mwanaume umezeeka kama kiporo sura inamichirizi hata maji yanakwama..haipendezi

Raha ya kuoa na kuolewa utembee na wako watu wakutamani na wamtamani kwa matunzo mnayopeana sio mchekwe barabarani kwa kushindwa kumtunza, unazani kulea mtoto wa mwanamke mwenzio au mwanaume mwenzio kwepesi kama kufunga khanga basi hata wa chekechea angelea kama wanavyojuwa kufunga khanga..

Somo zaidi hiyo tarehe 21/10/2012 wahi nafasi yako sasa shoga ukafundwe..

Lako hilo kama limekugusa..

Reactions:

2 comments:

  1. Shosti kwa kweli hilo neno.Lakin mimi ninachotaka kusema,wanawake tusikubali kushauriwa na waume zetu kuacha kazi.Wewe sawa atakuhudumia ,je ndugu zako ambao wanakutegemea?

    ReplyDelete
  2. Eeeh ndio wewe, unaetokwa na povu mdomoni hapo kwa kuongea na hasira kusema oooh shenzi sana hizi topic nyingine, lo oh inahusu kumfujisha mwenzio, na ulivokua huna haya kila kukicha unamtangazia aaah mwanamke yuko rafu sana, sio hadhi yangu, wakati hata lotion hununui, acha hzo gauni. Wajanja wanaojua kulea watakunyakulia ubaki kupepesa mijicho. Chezeeya jiji ww.
    Ni haki ya mwanamke kuhudumiwa na mumewe hata kama anafanya kazi huyo mwanamke.sasa mpaka sokoni waenda ww uliolea nn?? Maana ake nn nyumba ikawa na mwanamke ndani, ebooo!!! Basi muende wte achague na yy, mpaka vitu vyote wachagua ww, kaaah bwana una hila ww.

    ReplyDelete