Tuesday, August 7, 2012

Lako hilo JOTO hupati BARIDI maisha yako....

 Ucheshi tabia yangu ndivyo nilivyozaliwa, kucheka na walimwengu mimi nimeshazoea, sichagui yupi wangu binadamu wote sawa nakushangaa mwenzangu kisa cha kuninunia.

Sili chako nala changu acha kunipakazia, una wako nina wangu mbona unajishtukia???? kupendwa kipaji changu hilo kaa ukijuwa mpoozaji wa roho yangu yupo home katulia..hehe heiya

Wanitangaza ubaya mimi nisiokuwa nao, unasambaza umbea kuwaeleza wenzio eti nakuchukulia bwana wako tegemeo lako, wewe nakushangaa kusema maneno hayo, yupi wa kumchukuwa sijaona bwana hapo kama ukinichunia utaisoma namba yako.

Reactions:

0 comments:

Post a Comment