Tuesday, August 28, 2012

Hongera Connie shoga yangu kwa kutuletea kidume cha mbegu..

 guys sorry leo mtapata tabu kugeuza vichwa kuangalia hizi picha nimejaribu to rotate and saved lakini na shangaa kwanini zimekataa kugeuka anyways hii ilikuwa siku ya Connie juzi jumapili nyumbani kwake Kimara, ndugu na rafiki zake wa karibu walimchinjia kwa kumpongeza kujifungua mtoto wa kiume PRINCE  SAMSON

Hapo Connie alikuwa anatuhadithia heka heka zake alizopata wakati wa uchungu mpaka kujifungu


Prince (uuiii ni mzuri aje..) akiwa amebebwa na shosti huyo anaitwa Kiki ni mtoto wa shoga yangu Jacky na Mumewe PJ sijawahi ona mtoto wa kike amefanana na baba yake hivi mpaka sasa tumeamua kumita PJ sio Kiki tena...


Shosti zangu Connie hapo mwenye purple na Jacky mwenye khanga wakichekelea jambo kutoka kwa wifi wa connie..chezea wifi wewe..


Shoga yangu mwengine Amanda au mwenyewe anapenda kujiita kipenzi cha Jigge ameshika tama hapo akikagua mtori kama umepikwa vyema..chezea toto ya kichagga hapo karudishwa moshi kabisa
Kwa mbali pale ni connie na mumewe Anorld baada ya kupewa mabakuli mawili hatari ya mitori na chupa ile ilikuwa na kisusuio wanywe kama wazazi.. ni kawaida tu ya siye wachagga kufanya hivyo


Connie na mumewe walioketi, Jacky na mumewe PJ waliosimama


Wageni waalikwa...


Chezea mama mkwe wa Connie full kuomba hapa magume gume wachomwe kwa damu ya yesu yasipate kujishebedua na kujipendekeza kwa mwanagu wakamuharibia ndoa yake..


Chezea mashoga wa mama mkwe wa Connie wewe...wanawake wamewaka carrolite


Mama na Mwana


Hapa Connie alikuwa anakataa kunywa huu mtori eti bakuli kubwa alikuwa nasema nyie mpendeze miye ndio niwe kichekesho inahusu hanywi mtu hapa..sasa ungemsikia na sauti yake anachekeshajeee


Akalazimishwa huku akikasirika mbona aliunywa..

Mrs Mizizi na Mrs Mbonde


Mrs Mizizi and Mrs Jigge.. 


Chezea mama mkwe wa kihaya alikuja na mashoga zake kumtunza mwali alimvalisha hiyo head piece nyeupe na khanga 


Akampa na hivi vitu azidi kula na kujaa maziwa mtoto azidi kupata afya njema


Shosti akamkumbatia mama mkwe wake akimshukuru..


Mara BBM zikaanza kabla hata mama mkwe hajaondoka..Jamani


Wahaya sasa wakaanza kusakata rumba


Chezea wamama wa kihaya


Reactions:

0 comments:

Post a Comment