Friday, July 20, 2012

SOMO...

Jamani somo leo linahusu muonekano wako wewe mwenzangu baada ya kuwekwa ndani/kuolewa.

Kwanza kabisa nataka nitofautishe kukuwa kwa maumbile ya watu baada ya ndoa, kuna watu wengine maumbile yao baada ya ndoa uharibika baada ya kutumia njia za uzazi wa mpango, utakuta mtu labda anachoma sindano, ama anakunywa vidonge ama ameweka vijiti basi anafutuka ile mbaya hata akijitahidi kukonda vipi mtu haiwezekani.

Lakini pia kuna wale basi kwasababu kazaa atajiachia asingizie uzazi umemnenepesha inahusu???? asilimia kubwa ya wanawake wanapozaa kweli hunenepa lakini ni juhudi zako wewe baada ya kumaliza kunyonyesha ukajirudisha tena kwenye mvuto kama ulivyokuwa hujazaa.

Miye hapo nimezaa watoto wawili tena jumamosi na jumapili wamepishana mwaka na miezi saba, na mkononi nina kijiti cha uzazi wa mpango kwahiyo ningesema nijibweteke basi full kunenepa!!!! tambua urembo wa kwanza ulionao ni mwili wako, halafu ndio vitafwata hizo nywele, sijui kope, sijui kucha n.k

Utamkuta mwanamke jamani kanenepa kama nyumba, shepu yenyewe unakuta kama kabati huna upinde halafu umeolewa na mwanaume matata mtoto handsome boy wa mjini wewe umenenepeana mpaka mkiongozana anakwambia utangulie yeye aja nyuma kisa tu aibu ya kuongozana na wewe hehehe ya..inahusu  mkiwa chumbani kuchuma tunda mpaka akuweke sawa lisaa lizima anatafuta mlango wa kuingilia vizuri asije kujigonga, mpaka achambue nyama za mapaja huh...jamani haipendezi raha mtoto wa watu akitaka kuchuma tunda moja kwa moja anaenda uwanjani bibi pasafi, pananukia, mawaridi, mtoto kila kona ukigongwa unajibu akugeuze hapa, kule, mara hivi hachoki mtoto unabebeka hata akiamua kuchuma tunda kasimama kakubeba mtoto umo..sasa wewe ukiwa pande la mtu atakubeba vipi au ndio mpaka aite katapila...heheheh yako hiyo

Shoga uzazi, isiwe chanzo cha kujiachia, yani miye furaha yangu nipite sehemu kama si mwanaume mmoja hata wawili wageuke kunitizama mara mbili, unadhani hao wenye makalio makubwa na mahipsi tu ndio wanageukiwa!!!! wapi mwanamke mvuto babu hayo makalio hata ya kichina yapo ukiyataka ndani ya wiki unayo.

Nadhani utakuwa umenisoma..mwanamke upindo bibi sio unanyooka kama dira, unavimbiana kama biringanya, na ubapa kama kabati aihusu hata kidogo.

Reactions:

5 comments:

 1. mmh we rose embu acha kujisifia sana wkt ni kawaida tu mbn nakuona hivyo ulivyo ndo unazan watu watageuka kihivyooo wala, mi naona kawaida tu

  ila hilo la kunenepeana ni kwel jmn wanawake wengi wanajisahau wengine ht kuzaa bado ila utawaonea huruma walivyonenepeana ht shingo haionekan

  naona ni uhuru wanaokua nao baada ya kuolewa sijui maana anakula anachokitaka bac ndo anabugiaaa madhara yake ndo hayo sasa

  ReplyDelete
 2. mmh we rose embu acha kujisifia sana wkt ni kawaida tu mbn nakuona hivyo ulivyo ndo unazan watu watageuka kihivyooo wala, mi naona kawaida tu

  ila hilo la kunenepeana ni kwel jmn wanawake wengi wanajisahau wengine ht kuzaa bado ila utawaonea huruma walivyonenepeana ht shingo haionekan

  naona ni uhuru wanaokua nao baada ya kuolewa sijui maana anakula anachokitaka bac ndo anabugiaaa madhara yake ndo hayo sasa

  ReplyDelete
 3. Una maneno weye!!!!! Mi da Rose nina watoto wawili pia nakimbilia 37 years sasa...Lakini ukiniona utasema ni 25. Nafanya mazoezi mpaka push ups. Unajua mwili wa mazoezi unaongeza confidence. Nakumbuka nilipojifungua tu muda si mrefu niaenda kusoma ulaya...nikawa natumia makoti ya winter kama mkombozi wa kuficha tumbo maana kila aliyeniona alikuwa ananiuliza ntajifungua lini wakati mtoto tayari ana miezi 9...Nkasema ushenzi huu...nikaanza mazoezi...sasa hivi siwezi pitisha siku zijala tizi na mwanzo ilikuwa kama adhabu lakini kwa sasa nisipofanya mazoezi nahisi nimepungukiwa kitu.

  Ukinicheki kwa sasa mtoto shepu...mtoto guuu...paja limetulia halina nyama uzembe tena...nikipiga kimini mwenyewe najikubali. Tumbo lina misuli safi halijalegea ten...Hakuna short cut ...ni mazoezi na kupunguza ulafi

  ReplyDelete
 4. Raha jipe mwenyewe usisubiri kupewa na walimwengu..hehe heya mwanamke kujiamini bwana kuna dada knifurahisha sana mtoto gugu..shepu shepu lazima wa geuke..kama unajipenda jisifie na uupende mwili wako hata kama watu kikiwauma na kuwachoma ukweli ndio huo...umenisoma eeehh

  ReplyDelete
 5. Maza hausi hahahaha umenichekeshajeee...sio lazima wageuke kumi hata mmoja roho itamruka sasa mtu unakuwa kama sanamu la michelini, limegawanyika kwa matuta ya tumbo inahusu...haha

  ReplyDelete