Wednesday, July 11, 2012

SOMO..

Jamani somo leo nataka kuwapa wamama wenzangu, juzi nimekutana na rafiki yangu akawa ananiambia mumewe anafurahia tendo la ndoa zaidi akiwa na mimba kuliko akiwa hana, unajuwa kwanini, anasema lile jotojoto la mimba ndio lina mpa hamu ya kutaka kukutana naye mara kwa mara japo mkewe mara nyingi anakuwa hataki kwasababu ya kuchoka na maruweruwe ya mimba.

Nikampa siri moja ambayo na wewe mwanamke mwenzangu kama unatatizo na mumeo kama huyo shosti, wanaume hupenda kweli lile jotojoto lakini mimba haidumu milele, sasa basi ukiwa na mimba sawa na nivizuri lakini kama huna mimba nitakufundisha njia nyengine ya kuweka jotojoto kunako..ni kwakutumia udi

Sijui kwenu nyie lakini mimi ndani kwangu sikosi udi, na huwezi kuwa na udi bila kichotezo..siutumii tu katika kujifukiza nguo zangu bali na mwili pia, unafanyaje utachukuwa kichotezo chako siku hizi vipo vya kila aina mpaka vya umeme, weka udi wako juu pale kama unatumia cha umeme kipachike kwenye socket udi ujichome,ukifikia unapofuka moshi ukiwa kama ulivyozaliwa, na peke yako hata mumeo asikuone kwenye hili chuchumaa weka kile kichotezi chini kikilingana na anapoingia mumeo uruhusu moshi wa udi uingie ndani huku ukiwa umejitanda kanga ndio unaingia vizuri kaa hivyo kama kwa dakika kumi halafu toa, endelea kuacha udi uendelee kunukia ndani.

Hii ni nzuri ikifanyika wakati unajiandaa kukutana na mumeo sio aje masaa mawili baadaye ule ujoto utakuwa umeisha, akiwa labda sebleni anasubiri kuingia chumbani wewe fanya vile akifika hata baada ya dakika kumi bado lile joto litakuwepo, kwahiyo kama mumeo anapenda jotojoto fanya hivyo ulee ndoa yako unadhani kutunza mume kazi ndogo..shaurilo

TAHADHARI: kama mumeo ana allergy akisikia harufu kali anaumwa please usijifanye tena wewe ndio umefundwa ukamtoa mtoto wa watu roho, maana kuna wanaume wengine yani yeye mafua hayamuishi kamwe akisikia tu harufu basi atapenga na chafya hata mara kumi, hapo tena kutakuwa hamna raha bali karaha. umenisoma eehh

Nakwambia hivi mumeo atoke nje kwa tamaa zake lakini sio kwamba umeshindwa kumtunza, upo hapoReactions:

7 comments:

 1. Kama kuna kitu nachukia ni udi; kwanza nina aleji na harufu kali. Pili mina husisha udi na mashetani. Tatu hiyo njia mamito inaonyesha ni too artificial na kama ulivyokiri mwenyewe baada ya muda unapoa. Nne huyo mwanaume ambaye hajawahi sikia harufu ya udi ndani ya nyumba yake leo hii si atakuona unamwangia. Tujiamini wanawake we are hot no matter what. Kikubwa ni kuwa mtundu kwenye 6X6; hata akionja kwa wenye kutumia udi atarudi tu kwani atagundua wewe ni original si fake

  ReplyDelete
  Replies
  1. Kama wewe upo original shukuru mungu kuna wenzako ndoa zao zinawaka moto kama huyo dada hapo juu, mumewe kashasema anapenda zaidi kufanya naye tendo la ndoa wakati wa mimba kwasababu ya jotojoto sasa huo original ataupata wapi? mimi naona kama hiyo njia inamfaa na mumewe anaridhika aitumie tu aokoe ndoa yake, sio jinsi wewe unavyofikiria na majini ndio kila mtu yupo hivyo, basi majini yangejaa kiaribia kila nyumba

   Delete
  2. Kaazi kweli kweli ushamba kweli mzigo. Udi unatengenezwa kutokana na perfume hizi hizi tunazojipaka, sana sana unawekwa kutoka kwenye fomu ya kuweza kuuchoma. Kuhusuisha udi na majini au mashetani ni kichekesho kwa sababu kama wanapenda udi basi hata perfume nyingine zenye harufu kali watazipenda hivyo watu waache kupaka perfume.

   Mimi nanunua airfreshner Ulaya yenye scent ya udi tena imeandikwa OUD na ni brand kubwa tu ya wazungu inayotumia hiyo scent, sasa sijui wazungu nao siku hizi wanapenda majini? Kuwa muwazi dada tukusaidie vitu vingine mtavichukia bure kwa kuvihusisha na dini wakati havina uhusiano wowote.

   Udi ni perfume kama perfume yoyote ile uko unaotengenezwa na perfum kali na upo ambao ni mild. Na mimi nina allergy na perfum kali hivyo natumia ule wenye mild scent kujifukiza, na natumia airfreshner ya Oud ndani ya nyumba.

   Mwisho kama hujisafishi huko chini udi ni kazi bure, unatakiwa uwe msafi na utumie sabuni special kujisafishia huko chini na wala huna haja ya sijui kujitia vidole ndani, no ile sabuni tu kila siku ukioga unaitumia hiyo hutoi harufu kamwe!

   Delete
  3. mbona sie wanawake are so fake ni many ways??? hayo ma lipstic na ma makeup unayoyapaka upendeze ni still fake, au utajitia ni usafi. mbona ukitokwa na machunuSi au rushes usoni unakimbilia kutafuta kitu cha kutibi and you just dont say its natural since its just body changes taking place.
   jamani udi kwa mwanamke lazima na inategema na udi, hapa hatuongelei udi wa kihindi ule wa vijiti, mie personally siupendi. tunaongelea udi wa kujifusha mwanamke ukanukia hasa uko kunani.
   umemaliza siku zako, ndio wajiosha but harufu ya damu ni kali, jIfukize ka ulivoambiwa hapo juu tena ukiwa na maji maji ndo vizuri, kampe mumeo mambo, hata akienda chumvini mume mwanaume analamba atakavo maharufu ya periods haimpi distrubance yoyote.
   unamkatikia mwanaume jipapa linatoa uturi wa udi, sio chumba kizima kinabaki na harufu la papa, kaaah we wa wapi.

   Delete
  4. aksante tumtum wanikoshaga wewe hujui tu!!! nimejifukiza mie jana tu, ndo mara yangu ya kwanza, mume kuingia tu chumbani anasema mmmmhhh leo chumba chanukia vizuri, akaniambia daah natamani nyumba hii yote inukie hivo, nilifurahije sasa??? nakwambia mabusu nilompa mwenyewe akabaki kuduwaa, bibi mechi nimeicheza kwa raha zangu, mume anajienjy tu. leo asubuhi kwenye gari anantoleaje, mhh mke wangu jana hatari, sifa kibao. sasa nyumba yangu haiwezi kosa udi.

   Delete
  5. Anonymous 1: ni vyema kujitambua wewe kama mwanamke unapenda nini na kipi hupendi, na ukitumie vyema chumbani kwako panapojenga unyumba kama unaona udi haukufai basi mautundu yote peleka kwenye 6X6 kama ulivyosema ila udi ni chachandu tu inayonogesha kwenye hiyo 6x6..

   Delete
 2. Chezea tumtum wewe..hayo ndio mambo pwity pwity raha jipe mwenyewe shosti..loh halafu mtu ulie kila siku mume wangu anatoka nje ataacha kutoka kama ubunifu huna??? inahusu...hongera pwity kwa kumteka mumeo kwa kutumia udi..hahaha hapana chezea

  ReplyDelete