Tuesday, July 24, 2012

Afumania mke na mwanae, awaua...

Mkazi wa kijiji cha Ng'hoboko, Stephano Mihulu (60) anadaiwa kumfumania mkewe akifanya mapenzi na mtoto wao wa kumzaa na kuwaua kwa kuwakata mapanga.

Inasemekana, Stephano alimkuta mkewe akifanya tendo la ndoa na mtoto wake ndipo alipoghadhabika na kuwashambulia kwa kuwakata mapanga na kisha kuwachinja shingoni, baada ya kufanya mauaji hayo inadaiwa Stephano alitembea kwa miguu umbali wa kilometa 18 kutoka kijijini kwao na kwenda kujisalimisha kituo cha polisi cha wilaya hiyo.

Alipofika polisi alikabidhi silaha ambazo ni panga na fimbo alivyotumia kufanya mauaji hayo na kuwaambia alitembea kwanzia saa saba usiku mpaka asubuhi hiyo kwasababu hakutaka kuwasumbua polisi kwa kuanza kumtafuta.

Nimeipata: Habari Leo


Reactions:

0 comments:

Post a Comment