Wednesday, June 27, 2012

Masikini...

Dada Rose, natumaini wote humu ni wazima, lakini sio kwa upande wangu kuna siku niliwahi kukutumia email nikitaka ushauri kuhusu mke wangu, kuwa hapendi kukubali maisha aliyonayo na kutaka kuishi maisha ya gharama kama shoga zake, na mpaka akaenda kuchukuwa mkopo bila kuniambia ambao alishindwa kuulipa mpaka nilipomuwekea thamna na kumlipia, lakini mke wangu hakomi jamani yani ananivunja moyo kabisa wa kuendelea kuwa naye sijui kabisa nifanyeje maana nahisi sasa ni heri tu kuachana.

Baada ya kulipa ule mkopo wake na kumsema juu nikajuwa ya kwamba atabadilika na amejifunza kumbe nilikuwa natwanga maji kwenye kinu mwenzenu yaliyonikuta!!!!!!!! huyu mwanamke ameenda tena kuomba mkopo sehemu nyengine kama kawaida yake wala hakuniambia chochote na kama kawaida yake kashindwa kuulipa kwa wakati na sasa huku alipoenda kukopa wala hawakutaka kuja nyumbani kuongea naye kwanini hajaulipa.

Jumatatu nilipotoka kazini nafika nyumbani nakuta nyumba tupu, hamna makochi,hamna Tv, hamna radio, hamna friji yani nikabaki nimeduwaa kwani tumeibiwa mchana vitu vyote hivi, mke wangu hata sijamkuta nyumbani namuuliza msichana wa kazi ananiambia watu wamekuja wakaamwambia mama tumeamuriwa kuchukuwa vitu wakavibeba na kuondoka.

Alivyoniambia tu hivyo nikajuwa moja kwa moja ni mambo ya mkopo, yani niliumwa tumbo ghafla kumpigia simu hapokei na yakuudhi zaidi siku hiyo hakurudi nyumbani..ni afadhali lakini maana ningemuua akarudi kesho yake kwa magoti akiwa na dada yake, analia anaomba nimsamehe jana hiyo sasa, sijamjibu lolote maana sijaona lolote la kuongea naye nampaka sasa nipo kazini sijui niongee naye nini maana hata hamu naye sina, kama unaweza fanya mambo mpaka yatokee hivi huyu mwanamke si anawezaniua dada????? sina hamu naye kabisa sijui kabisa nifanyaje mwenzenu

Shukrani

6 comments:

  1. muache haaka. ndo tabia yake hatowacha. iko siku utatembea bila nguo kisa madeni ya mkeo.

    ReplyDelete
  2. Pole sana kaka. Haya yameishatokea tayari. Kwa sasa kaa chini na anza jipange upya. Kama unaona bado una hasira naye mwambie aende kaa kwa dada yake mana hasira sazingine zinaweza kupeleka na ukamfanyia kitu kibaya. Take courage, huyo ni mkeo. Yaliyotokea yamekwishatokea msamehe na muendelee na maisha.

    Nakushauri usali sana ili kulainisha moyo wako. Hii itasaidia katika kujenga ndoa yenu upya. Msamehe tu mkeo mana tayai anajutia yote aliyoyafanya. Pole sana.

    ReplyDelete
  3. haaichi huyo kashazoea. mpige chini.

    ReplyDelete
  4. Mwambie akarudishe vitu vyote vya humo ndani mwako ndio na yeye aweze kurudi. Atajua mwenyewe atafanyaje kama hao ndugu zake watashangishana pesa shauri zao, kwa sababu haiwezekani dada mtu alale na mdogo wake kwake huku akijua ni mke wa mtu. Kuwa na msimamo mwambie nataka vitu vyangu vyote virudi ndio na wewe urudi humu ndani. Kwa njia hiyo labda anaweza kukoma, lakini ukimsamehe hivi hivi tu, atakuweka rehani hata wewe mwenyewe.

    ReplyDelete
  5. Kaka dalili ya mvua ni mawingu, ulishayaona mawingu na sasa mvua imenyesha bado unajiuliza uliza tuuu maswalii, cha muhimu ni arudishe hivyo vitu kwanza ndio muanzie hapo kusameheana maana mara ya kwanza ulisawazisha na sasa mara ya pili unaongelea kusamehee, hata acha huyo kashazoea.
    Na pili je unajua hizo pesa alizokopa zimefanyia nini?? maana hayo ndio maswali ya kujiuliza na sio kukurupuka tuu, aseme ziko wapi maana uwe mwangalifu kwa matumizi ya hizo pesa, angalau kama atakuonyesha kitu kulichopatikana kutokana na hizo pesa.

    ReplyDelete
  6. Mi nadhani cha muhimu ni kujua hivyo vitu nani kavichukua. Maana kisheria huwezi kuweka dhamani mali isiyo yako. Fuatilia vimepelekwa wapi wakurudishie vitu vyako, watajuana namna gani atawalipa. Yani mi TV yangu afu mtu aiwekee colateral waje waibebe mbona watanitambua wawe Pride sijuhi FINCA sijuhi upuuzi gani; huwezi chukua kitu cha mtu ambaye si mkopaji kulipia deni period.

    ReplyDelete