Tuesday, May 29, 2012

Ndoa inapokuwa chungu...

Kwanza kabisa mada ya leo inahusu dini ambayo utaratibu wake wa kuoa siujui vizuri ila kwa wale waislamu naomba mtueleweshe vizuri maana kuna mkasa mmoja ambao umemtokea rafiki yangu wa karibu ambao leo nataka niwaeleze na nyie mumpe na ushauri hii nimehadithiwa jana jioni.

Huyu dada anaitwa Asila, yeye yupo kwenye ndoa mwaka wa pili anautafuta wa tatu na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike, huyu dada na familia yake wanakaa kimara, ni waislamu japo mwanamke sio swala tano lakini mumewe ni wa aina hiyo kwani pia ni ustaadhi(natumaini nitakuwa nimepatia).

Dini hii kwa tunavyofahamu inaruhusu mume kuoa wake mpaka wa nne, lakini kwa mume kuomba ruhusa kwa mkewe wa kwanza na kumhakikishia kwamba anamudu kutunza mke zaidi ya mmoja na pindi atakapokubaliwa na mkewe ndipo anapooa mke wa pili na kuendelea na ninasikia mke mkubwa anakuwa na sehemu kubwa sana kwenye hiyo ndoa ya mke mdogo mara nyengine hata kushona sare na bi harusi.

Sasa basi Asila yeye kabla hajaolewa alikuwa sista duu balaa hakuna top wala mkato wa suruali uliingia hapa mjini bila kuwa nayo, mpaka alipoolewa na huyu kaka kwa harusi ya kupangiwa na wazazi kwakuwa waliijuwa familia ya mumewe na baada ya kuolewa alitakiwa kuachana na mavazi yale na kuwa mke wa ustaadhi kujitanda, kuvaa nguo za heshima na kutosahau juba wakati wote.

Kwakuwa alikuwa kwenye ndoa alifwata masharti yote na mumewe japo alikuwa hampendi kwasababu alikuwa hajawahi kukutana naye mwanzo lakini kwasababu jamaa alikuwa na hela sana basi haikuwa ngumu kujifunza kumpenda kwakweli yule kaka kwakumuhudumia mkewe kweli hata sisi rafiki zake tulimtamani style yake, maana japo alikubadilisha jinsi ya kuvaa utamkuta anabonge la juba lakini mtoto alikuwa akisukuma prado ya hatari, alivaa vya gharama, yani gold hizo kwake ndio balaa nakumbuka siku nilimpeleka mwenyewe kununua ya kiuno Shs M 1na sio vitu tu na mumewe humpa hela ya matumizi kwa mwezi Million moja ya kwake tu sio ya matumizi ya nyumbani,  huko nyumbani kwake ndio balaa yani kwakweli anamaisha ambayo kila mwanamke anatamani kuwa nayo.

Miaka miwili na nusu sasa kwenye ndoa, mwanamme hajabadilika kumuhudumia mkewe wala kumuonyesha mapenzi ila mumewe akaja kuoa nje mke wa pili, bila hata kumuarifu mkewe yani ameoa mkewe hata dalili hajaona kila kitu kilifanywa na ndugu wa mume baada ya wiki tatu ndio mumewe anamueleza Asila kwamba ameoa huko kibaha na kwasasa amemnunulia mkewe (mpya) nyumba kimara anataka amuhamishie huko ili awe naye karibu!!!!!!

Asila ananiambia alihisi kasikia vibaya, akamuuliza unasemaje? mumewe akarudia tena maneno yake na ndipo akaamini hakusikia vibaya..anasema alisikia kama kuumwa tumbo la uchungu kwa muda akaanza kuwaza amewezaje kufanya hivyo bila ruhusa yangu alipo muuliza mumewe alipewa jibu ambalo kwa dakika ilimfanya amke kwenye starehe alizokuwa akipata na kukumbuka huyu kaka hakuwahi hata kumjuwa kabla hajamuoa. Mumewe alimuuliza kwani tokea nimeoa umepungukiwa nini? siufurahi nimeoa kuliko ningekuwa nakusaliti kwahiyo uelewe unamwenzako ukiona sijalala ndani ujuwe nimelala kwake.

Asila ananiambia siku hiyo hakulala aliingia chumbani kwa mwanae alilia karibia usiku mzima akawa anawaza amfanyaje mumewe yeye kwake hakutaka kujuwa kama dini inaruhusu anasema akaanza kuwa hamfanyii mumewe lolote akija anamuachia dada (nikamwambia sasa ataolewa dada na wewe utaachwa) akasonya...

Ushauri wangu kwa Asila nikamwambia kwa ilipofikia huwezi kubadilisha chochote, najuwa inauma sana mumeo anapokuwa na mtu mwengine na asikuambie mmtu penzi aligawanyiki lazima kunammoja atakuwa anadanganywa yani aje kwako kwa mapenzi na kesho kwa yule kwa mapenzi miaka yote kunakipindi itafika mtakuwa wote kama ndugu hakuna mwenye wivu wala na mapenzi na mwenzie kama mwanzi.

Sasa basi hakuna kuondoka madhali kila mtu ana kwake shida ya nini na uzuri mumeo bado anakuhudumia bado unapendeza shida kitu gani (akaniambia akiwa na hamu ya tunda halafu mumewe hayupo atafanyaje ama achume nje) hapo nilikosa la kumjibu nikamwambia angekuwa hakuudumii ningekwambia la kufanya lakini wajibu wake kama mume na baba anautimiza hamu ya siku moja ama wiki ndio ikufanye utoke nje?

Hayo ni mawazo yangu sijui wewe..na nilimuhakikishia nitaiweka story yake hapa kama utachambwa utaniwia radhi



3 comments:

  1. ww dada ww n muislam na unajua dini inaruhusu mumeo ingawa alitakiwa kukwambia lkn atakuwa aliona kuwa akikwambia hutakubali ndo mana akafanya kimya2 ILA SBB HAPO ULIPO HUJAPUNGUKIWA NA KI2 NA MUMEO BADO ANAKUTUNZA YAN HAMNA SHIDA YYT BAS TULIA MANA HUNA JINS HATA UKISEMA UMUACHE UTAPATA WAP MATUNZO KM HAYO DUNIA YA LEO WATU WANATAFUTA BAHAT KM HYO HAWAIPAT, TULIA ILA HELA UNAZOPEWA UWE UNAJIWEKEA AKIBA ILI LIKITOKEA LA KUTOKEA UWE NA PAKUANZIA, NINGEPATA HYO MIJIHELA MIE MBONA NINGETULIAAA, ALAF HYO HAM ATAKUJA TU KUITULIZA MAANA HAWEZ KUKAA KWA MKE MWNGNE ZAID YA WIKI.

    J.

    ReplyDelete
  2. Mimi nakujibu kama mwanamke wa kiislamu, mwanaume hatakiwi kumuomba ruhusa mke wake ili aoe mke wa pili, kwanza ni mwanamke gani atatoa hiyo ruhusa? Hiyo ruhusa wao wamepewa na Mungu ila kwa sharti la kuwa wawe waadilifu, na kama mwanaume anajiona hawezi kuwa muadilifu (yaani kuwatendea sawa sawa wake zake wote) basi aoe mke mmoja.

    Na kama mke anaona kwamba nafsi yake hawezi huo uke wenza basi anaruhusiwa kwenda kwa kadhi (hapo ndipo linapokuja suala zima la mahakama ya kadhi) na kutoa Khula (kumpa mume talaka). Na talaka hii au kujivua huku kwenye ndoa sio lazima iwe kwa suala la uke wenza tu, mwanamke anaweza kutoa Khula iwapo anateswa, ananyanyaswa au hatimiziwi mahitaji yake muhimu na mume.

    Tukirudi kwa shogako inaelekea hiyo ndoa haikujengwa kwenye misingi ya mapenzi, bali kwa matakwa ya wazazi. Huyo mume alioa kuwaridhisha wazazi wake hali kadhalika mke alifanya hivyo hivyo. Pamoja na yote hayo hawakuwa na muda wa kujenga mapenzi baina yao. Kila alichokuwa anakifanya mke ni kwa ajili ya mali, na hata kuacha kutembea bila kujistiri amefanya kwa ajili ya mali ya mume na si mola wake. Na majibu ya mume yanaonyesha kuwa hana mapenzi kwa mkewe ndio maana anakosa busara kwenye majibu yake. Cha msingi anaweza kuamua kuondoka au akaamua kuendelea na maisha ya ukewenza lakini atafute kitu au shughuli zake za kufanya kwani mwanamke wa kiislamu anaruhusiwa kuwa financially indipendent.

    Kuhusu suala la kugawanyika kwa penzi unataka kusema wanaume wa kikristo hawana mahawara na vimada nje ya ndoa ilhali wanawapenda wake zao?

    ReplyDelete
  3. Hiyo ndio faida ya kuoana kwa kufuata mali, ndoa haina mapenzi. Ndoa yenye mapenzi ya kweli ingekaa hata miaka 6 kabla mume hajafikiria kuleta mke mwingine, inaelekea kuna kutokuelewana baina yao kulikopelekea mume kwenda kutafuta utulivu kwa mke mwingine. Ingekuwa mkristo angekwenda kutafuta nyumba ndogo.

    Wakati mwingine wanaume wengine hawatosheki tu sexually na anakuwa anataka kila siku, sasa ukijitia unachoka ndio anakwenda kutafuta mwanamke mwingine wa kumtimizia. Ila sasa kama ndio ishatokea mara nyingi kipya kinyemi, ingekuwa mie ningemwambia kakae huko uinjoy tani yako hata miezi 6, hamu ikikuisha ndio urudi. Mara nyingi mtu wa aina hiyo baada ya miezi 6 na huko nako anakuwa kishachoka. Na kama uko smart anaweza kurudi mwenyewe taratibu kuliko kuanza kushindana. Na kama ulikubali kuolewa kwa sababu ya mali na mali anakupa what more do you want? Hata angekuwa si muislamu bado usingekuwa peke yako. Wanawake wengi wanashea wanaume siku hizi labda uamue kuwa single.

    ReplyDelete