Tuesday, May 15, 2012

Hata Hiyo Mahari Nisingelipa...

Hivi dada Rose mimi nashindwa kuelewa kwanza kwanini mtu akitaka kuoa lazima alipe mahari? kwanini tusingekuwa tu tukionana tukapendana na kuamua kuoana then tuwataarifu tu wazazi na tuoane hii mahari ni ya nini? na siku hizi mahari zimekuwa bei juu sana kama mimi wakati naoa mahari ya mke wangu ilikuwa millioni moja yani mpaka unashangaa kupendana mpendane nyie halafu tena na mahari nimlipie ili niwe naye milele na kwanini nimlipie yeye tu na siyo wote tulipiane situnaenda kukaa pamoja? haya rafiki yangu wakati anaoa mahari yake ilikuwa millioni moja na nusu miaka miwili ya ndoa kagundua mkewe wajanja wa mjini wanamsaidia jamani huku sikutaka kuuana? maana jamaa kwa jinsi alivyoumia mpaka akakumbukia maharai yake aliyolipa bila hata kubakisha halafu mkewe pia wanamsaidia inauma sana
Mimi naona tu hii ishu ya mahari isiwepo kabisa maana sasa itafikia wanaume wakitaka kuoa wanaanza kwanza kuuliza naweza nisikulipie mahari ama ndio kutakuwa hamna kuoana bali ukipata unayempenda unavuta ndani mnazaa habari imeishia hapo.

Ahsante

Reactions:

2 comments:

  1. kaka mpe pole sana rafiki yako lakini kuhusu mahari kuwa kiwango cha juu inategemea famillia hizo mbili zilivyo elewana, na hii kulipa mahari ni kama kuwaambia wazazi wa mkeo asante ni bahati mbaya tuu baadhi ya makabila hapa Tanzania wanafanya mahari kama mtaji, ila kinachotakiwa ni kama kutoa asante tuu,na hii ya kuhusu mahari si lazima iwe pesa ni kitu chochote unachoweza, hata katika bibilia yakobo alifanya kazi ya kuchunga kondoo wa baba mkwe wake miaka saba ikawa kama mahari yake kwa ajili ya kumuowa Rahel japo alipewa Leya ikabidi afanye tena kazi miaka mingine saba,(MWANZO 31:15 kuendelea) kwa hiyo ichukulie mahari kama shukurani na sii biashara kama wengi wanavyofanya.

    ReplyDelete
  2. Mh! kusema kweli mahari siku hizi ni balaa tupu, mimi dada yangu kalipiwa milioni na nusu, sasa najiuliza mimi wakati wangu ukifika nitalipishwa shilingi ngapi? Mi nadhani siku hz mahali inatumiwa vibaya kuna uchakachuaji nchi imeshaoza kuanzia viongozi mpaka familia huku chin. Kaka mi nadhan swala la mahari liwe la kutoka vitu vidogo vya kimila kama ilivyokuwa zamani, Blanketi, Mashuka, Mbege ... na kwa kawaida isiwe kubwa iwe wastani mfano ikiwa kama laki2 moja na nusu si mbaya sana, sasa mamilion kwa siku hizi, kwa kweli kwa mpango huu mbishe msibishe ndio maana siku hz watu wanavuta tu wanawake na hawaoi kama zamani kwanza watu wanataka harusi kubwaaaaaaa, pili mahali inayopangwa ni kubwa pia so watu wanavuta kimya kimya. Aizoo hapa wa East Zu! Dodoma

    ReplyDelete