Monday, March 19, 2012

SOMO......

Somo leo nalipeleka kwa wale wangosho kutwa wao kuingilia mapenzi ya watu, na kusema maneno kibao kwa watu, yani utakuta fulani na fulani wanataka kuoana basi wewe kwavile yule ulikuwa unamjuwa labda alikuwa mwanaume wako ama mwanamke wako unatembea kila mtaa kuzungumza mambo yake ya nyuma yasiyo kuhusu...unataka olewe/ kuoa wewe lililokushinda mpaka akafwatwa yeye lipi, huna ujuzi nenda ukafundwe.. haipendezi

Kama kaamua kumuoa ama kuolewa na yule kwani wewe hakukuona oohh alikuwa anioe mimi inahusu mbona kakutema, nyoo huna aibu, jitu zima likivua nguo watoto wanakimbia unajilegeza kutoa maneno yasiyokuhusu utasutwa na harudi kwako kashakutema kaoa/kuolewa kwa mwengine wewe kwako ilipendwa hata ujishebedue vipi harudi tena kwako..nazi mbovu wee iliyokamaa ikakosa pakujishikiza na kudundokea kwenye shimo la taka kila atakayepita anaitemea mate...utaisoma hii..chezea vyeupe ndugu hivi vyekundu vitakutia doa.

Tena mkome kabisa maneno unayapeleka kama mchawi, mara mtoto wa watu kaugua presha akifa utamla wewe nyama, ama utaikata m.....o/a yake uitunze ndani? ushatupwa kule wewe hunajipya wakati wa mwengine huu muache ajilie vyake kwa raha zake.

Utakuwa umenisoma..
Reactions:

2 comments:

  1. shost nani huyo amekuudhi hvyo?

    ReplyDelete
  2. weraaaaaa weraaaaaaaaa hahahahahahah nasikiaje raha jamani, yaani wewe amabe una tabia hiyo koma, tena na ukomae, haihusuu kabisaa, kwani hata kama kashatembea na wewe nn cha ajbu sasa hivi yuko na mie na kashanioa?? hehehehe haijalishi kitu mie ndo alonitukuza na kaona nafaa akaniweka ndani, we hapo ulikua njia tu kila mtu atapitia.
    umeisoma eeeh?? unalo hilo. tuache sie tule vyetu. kwanza nakuombea maisha marefu upate kuona zaidi tunavyokula vyetu vitamu. usije kufa wewe na presha!! hatuachani ng'oo, ndo kwanza tunazidisha!!

    ReplyDelete