Friday, July 8, 2011

UNANDOA UNALALA NA JEANS INAHUSU????????

unajuwa wakati wa kulala ni wakati wa kupumzika haswa baada ya siku ndefu, na unapolala hutaki kusumbuliwa haswa kwa mavazi ya kulalia hutaki kulala na kitu ambacho kinakubana, haswa kwenye ndoa tumeshaambiwa ya kwamba sharti la kwanza la ndoa ni kulala bila nguo unalifahamu????


na tunajuwa raha ya mapenzi ni nyama kwa nyama yani na maanisha raha ya kulala na mpenzi wako akikukumbatia ushtuke maana nyama zimegusana, na tunajuwa hakuna ndoa yenye raha muda wote kwani ni milima na mabonde kama anavyoniambiaga mume wangu..


sasa wewe mwanamke unagombana na mumeo wakati wa kulala unamvalia jeans jamani inahusu? wakati muda ule mliogombana mapenzi ndio yanakuwa matamu ama hujui njia nzuri ya kumaliza mgogoro ni kwenye sita kwa sita sasa wewe kulala na jeans unamahanisha nini usiguswe?????


jamani haipendezi haya kama umeamua kulala na jeans kwanini mkipatana unavua nguo, bwana maziwa yatabaki maziwa na tui litabaki tui, mwendo ni mmoja tu mgombane msigombane mpenzi kuona paja kupo pale pale kisa cha kumnyima mtoto wa watu raha ya kuoa, maana raha mkilala akupapase ajibembeleze mpaka alale sasa wewe unamvalia jeans kisa cha kumchubua vidole mtoto wa mwanamke mwenzio,, shosti aihuuuuuuuuuu kabisa....

Reactions:

1 comments:

  1. Wanawake wengi wanadhani kumnyima unyumba mumewe ndiyo njia pekee ya kumkomoa. Lah hasha, hiyo ni njia ya kuongeza ugomvi na matatizo katika ndoa. Tendo la ndoa ni msuluhishi mzuri kwa wanandoa. Kama mmegombana kwa kiwango chochote kile, lakini mkashiriki kwenye tendo la ndoa, hakika hapo hakuna tena ugomvi! hiyo sasa itakuwa tu ni vijimamneno vya hapa na pale na hatimaye mambo yatakuwa shwari. Hivyo, wewe mwanamke usitumie njia hiyo ukidhani utapata suluhu katika matatizo yako na mumeo. Je, ukimfanyia hivyo naye akasusa jumla utafanyaje? utaanza kujilaumu kwa hili na lile na wale mwenye imani potofu wataanza mambo ya kishirikina.Zaidi ya hayo, ndoa ni uvumilivu. Hata kama mumeo kakukosea usimnyime unyumba, wewe mpe ndoa kama kawaida na wakati wa tendo hilo unaweza ukamweleza mumeo mambo ambayo yanakuudhi na hivyo anaweza kujirekebisha.Wanawake mlio kwenye ndoa acheni kubweteka! siku hizi kuna ushindani mkubwa katika kila kitu! ukisusa wewe kumpa wengine watampa na baadaye utajiona mjinga!

    ReplyDelete