Wednesday, July 6, 2011

KUTOKUTAIRIWA KWAKE KUNANISUMBUA MIMI...


mwanaume wangu ni kijana wa maana sana ukimuona kwakweli anavutia sana yani hata mimi nilivyomuona mara ya kwanza kabla hajanitamkia kunitaka kimapenzi nilashamkubalia lakini pamoja na uzuri wake na utanashati alionao mwanaume huyu anakasoro ya kitu kimoja jamani..

mwanaume wangu huyu hajatairiwa, anasema kabila lake mwanaume akitahiriwa anakuwa anapunguza heshima ya uume yani mwanaume kamili kwao ni yule ambaye hajatahiriwa!!!!!!! kwakweli kwasababu mwanzo tulikuwa tunatumia condom wala haikunisumbua na ukiangalia anajuwa kweli kunimudu...

miaka miwili sasa imepita bado tupo pamoja ni juzi tu tumeanza kulala bila condom kwasababu tumeamua kutafuta mtoto ili tuoane nikiwa mjamzito kasheshe ni kwamba anakuwa ananuka, yani tukimaliza lile tendo anakuwa hajisafishi vizuri mpaka mimi ni msafishe saa ingine tukiamua kukaa na kuchunguzana mwili namkuta ndani ya gozi kuna utandu mweupe kwakweli unanifanyanisikie vibaya sana.

nimemshauri ya kwamba twende akatairiwe lakini hataki, jamani hapa ni mjini namwambia huko kijijini atajuwa nani umetairiwa lakini yeye hataki, sasa nitamsafisha mpaka lini sawa sio kazi kwangu lakini siku nyengine nakuwa nimechoka ama nitakapo beba ujauzito itakuwaje nikishindwa kumsafisha..

hii si aibu!!!


Reactions:

2 comments:

  1. Huyo bwana ni Mjaluo, maana wajaluo ndio hawatairiwi.
    Nilidate mtu na alikuwa anakazi nzuri sana. Lakini uchafu wake ulinishinda. Mwanaume alikuwa hajui kujisafisha kabisa mpaka nilikuwa najiuliza akienda kuoga huwa anafanya nini huko??? Ukimuona kwenye Suti utadhani ni msafi sana kumbe yote hiyo ilikuwa juhudi yangu, lakini nilichoka. Mwanamke utamani usafi wa mwili mtu ajifanjie mwenyewe huko akioga, lakini sio akitoka uko uone vitu vya ajabu hata sex hautaki tena. Nilimuacha nipata mtu mwingine ambae sina haja ya kumsafisha.

    ReplyDelete
  2. Kwa kutambua tatizo hilo ambalo pia linachangia maambukizi ya UKIMWI, Serikali imeanzisha Mpango Maalum wa kutahiri wanaume ambao hajafanya hivyo. Mpango huo upo katika mikoa ya Mbeya, Mara, Kagera, Mwanza, Shinyanga na pia Tabora.Ngugu zangu walengwa,msiogope kama bado haujatahiriwa. Nenda hospitali utaondolewa hiyo ngozi ya ziada na utaondokana na hiyo adha ya kuupekua pekua kwa ajili ya kuondoa huo utando. Ni uchafu usio na mithili! Pia katika tendo la ndoa hutasikia raha kama ilivyokusudiwa. Uume wako unatakiwa uwe kama "mkuki" siyo kama unataka kuanza shughuli uanze kuvuta nyuma hiyo ngozi iliyozidi. wengine wanasema mkono wa sweta. Aidha, ili kuondokana na tatizo hilo kwa siku za baadaye, Wazazi wote wahakikishe wanawatahiria watoto wao wangali wadogo. Hata hivyo changamoto iliyopo ni kwamba, Je, wazazi ambao hajatahiriwa watapenda kuwapeleka watoto wao kwenda kutahiriwa? hawataona aibu na fedheha?

    ReplyDelete