Friday, May 6, 2011

KANIPA TALAKA, MAMA MKWE HATAKI NIONDOKE..




Japokuwa ni mwaka wa sita wa ndoa yangu na sijabahatika kuzaa sio sababu ya mume wangu kuninyanyasa, ndani ya miaka sita ameshazaa nje na sasa anataka kuoa mke mwengine...


kwakuwa sisi waislamu dini yetu inasema ni lazima akupe talaka ndio akuache ama uridhie mwenyewe kuletwa mke wa pili, yeye aliponiuliza mimi nikakataa kuletewa mke wa pili ndani (tumepanga chumba kimoja) nikamwambia kama ni mtoto siumeshazaa nje sasa unataka kuoa msichana mwengine na chakushangaza hakumwambia huyu msichana mwengine kwamba ameoa kwake anasema kwamba mimi ni dada yake..


kinachoniuma mume wangu anaongea naye simu za kimapenzi nikiwa humo ndani mwetu anamueleza jinsi anavyompenda na kumwambia yeye ndio mama wa nyumba yake, nikimuuliza kwanini anafanya hivyo ananipiga na kunitukana na kuondoka kulala na kulala nje (ndio anakuwa amepata sababu)...


nimemwambia kama anataka kuoa basi anipe talaka, ameandika talaka na anasubiri tarehe aliyopanga na mshenga wake anipe lakini mama mkwe wangu ananiambia hata akinipa talaka nisiondoke kama mume wangu anataka kuoa mke basi ahame yeye aniachie kila kitu akaanze maisha mapya na huyo mkewe...kitu ambacho mume wangu sidhani kama atafanya mpaka naogopa.....


tarehe kumi na tano ndio siku yao ya harusi sasa nawaza sijui atanitimua nje, ama nibaki na mimi nikomae mpaka nimuone huyo msichana nimpe wazo kuhusu mumewe kwamba ni mtu wa kuoa na kuacha(kisa yeye muislam halisi hali haramu akitaka lazima aoe)....


nikisema niondoke mume wangu hataki nichukue chochote, baada ya miaka sita nitaanzaje upya?

4 comments:

  1. Kuna watu wengi wamepitia hiyo na bado wanaanza upya, maisha ni mafupi sasa wewe unangangania vitu vya dunia na ukifa na pressure bado utamwachia huyo mama. Ni afadhali uviache na kuanza upya, mungu ana miujiza na unaweza ukapata kila kitu chini ya mwaka mmoja na ukaendelea na maisha. Kuzaa ni majaliwa, kuolewa ni sheria, usipopata vyote usikufulu.

    ReplyDelete
  2. pole sana kwa hayo yaliyokukuta. yaani nilivyosoma hii story yako nimesikitika sana. mimi naona bpra uondoke hapo kwa mumeo, i hope ndugu zako wanakupa support. huyo mumeo atakupa presha tuu ukiendelea kukaa hapo. kwanza ukiangalia mmepanga chumba kimoja. hiko chumba na vitumuachie yeye na huyo bingti atakaemuoa. muombe mungu sana, kwani mungu amesema ukiniita nami nitakujibu. mungu anakuona unavyoteseka katika ndoa yako, lakini mumgu ndio atakaelipa kila kitu.
    nasema pole sana. mungu yupo pamoja nawe.

    ReplyDelete
  3. Pole sana dada yangu,hata mie yalinikuta kama yako ila tofaiti mie nilizaa ila tatizo lilikuwa ni kabila,niliondoka nikienda kuanza maisha mpya. Ila kabla ya yakuondoka niliswali sana na kumuomba mungu anisaidie kweli mungu hamtupi kiumbe cha na kama kweli huna makosa,nilianza maisha kwa ugumu sasa hivi nimepata kila nilichomuomba mungu tena zaidi yake yeye mpk anaomba turudiane na yule mke walishindwana akaondoka. Simtaki hata kumuona,wewe hutoka hapo kwake nakuhakikishia mungu yupo pamoja nawe.

    ReplyDelete
  4. Umepewa comments zote hapo juu, dada yangu kimbia sasa. Maisha ni mazuri tu, mungu atakupa vingiiiiiiiiiiiiiiiii kuliko kukaa kwenye hiyo ndoa.

    ReplyDelete