Friday, April 22, 2011

HATA AHANGAIKE VIPI SIFIKI KILELENI...

ni mwaka sasa tokea nipo na huyu mpenzi wangu, kwakweli kijana amekamilika katika kila idara lakini siyo ya sita kwa sita, anamapenzi ya dhati kwangu na mimi najuwa hilo, ananihudumia kwa kila kitu nitakacho yaani ni mkaka mtanashati sana lakini tatizo lake ndio hiloooo....


mara ya kwanza nilijuwa labda ni bahati mbaya tu kwa kuwa ndio tunakutana kwa mara ya kwanza ya kwamba anauoga lakini ni mwaka sasa na ngoma ni ileile nimeshaliongelea kwa rafiki zangu wakanishauri labda niwe nachukuwa muda sana mpaka kukutana naye kimwili labda wiki tatu ama nne ili kila mtu aweze kuwa na hamu na mwenzake labda itasaidia yeye kupata nguvu ya kukufikisha juu.... lakini wapi jamani hakuna lolote lililobadilika


watu wengine wanasema labda ni ugonjwa anahitaji tiba ya vyakula fulani, inawezekana kuwa ni ugonjwa ama uvivu wake tu wakutotaka kujuwa na kuniuliza afanyaje ili afike? maana nimeshamwambia na yeye ananiambia tu "baby ninachoka na mihangaiko ya siku nikifika kitandani nashindwa kabisa, ndio maana nawahi kufika kabla yako na kukosa nguvu ya kuendelea"...

nahisi kutaka kumuacha lakini nampenda sana, sasa huu ugonjwa jamani unatiba ni kweli kuna hivyo vyakula ama tuwe tunalala siku ambazo haendi kazini maana maisha kama haya nahisi huko mbele yatakuwa magumu kuyavumilia...

2 comments:

  1. Jamani sisi tulionahao wenye kututimimizia lakini hawana pesa wala kututunza, tunataka mwanaume mwenye kuwa na responsibilities na wewe unataka kumkimbia! mapenzi ya kitandani wengine tulidhani ndio yatalipa bills sasa najuta. Mwanaume wa kuomba pesa kila siku, haya sasa wewe ndio unayoyataka hao. Karibu kwenye club, wengine yametushinda.

    ReplyDelete
  2. Dada yangu kitanda hakinunui chakula wala kulipa umeme! fikiria sana hili jambo kabla haujaenda mbali. Mwanaume mwenye kutunza nyumba na mwenye kukuridhisha kitandani ni vitu viwili tofauti lakini wa kitandani mtapata therapy itapona, wa kuombaomba pesa kila siku na kutaka kutunzwa utamchoka mwishowe!

    ReplyDelete