Sunday, February 27, 2011

NIMEKUOA WEWE AMA NIMEOA UKOO WENU????????

jamani wame kuweni makini sana na wake zenu, hivi wewe baba leo unataka kuoa halafu unavyomfwata mchumba wako labda mmekuwa wote muda mrefu ama mfupi na kumuomba umuoe ili mtunze familia yenu ya watoto Mungu atakaowapa...

halafu baada ya ndoa wewe baba ukakusanye ndugu zako waje kuishi na nyie jamani inahusu, ama kisa wewe umeoa kwahiyo unadhani unamamlaka ya kutunza watoto wa ndugu zako na mkeo, kisa yupo atahakikisha wana afya nzuri na wanavaa vizuri!!!!!!!!!!!!!!!!

inamaana usingemuoa huyo mkeo hao watoto wa ndugu zako wangekufa???? ama wangekuwa wanapata wapi matunzo????? halafu sasa hao ndugu zako walivyokuwa hawana adabu, na kazi ndani wala hawamsaidii mkeo ukikuta nyumba safi na chakula mezani ulishawahi kumuuliza mkeo aliyepika na kufanya usafi ama hao ndugu zako wameletwa kuwa pambo la ukoo wenu??????

ukielezwa matatizo yao unajiuma uma huna maamuzi ya maana, sasa mkeo kakuoa wewe ama ukoo wenu, nyumba haina raha haina amani mara huyu kafanya vile mara yule hivi chakula bila kilo mbili kwa siku hamjashiba sio mchana wala usiku kisa cha kumuotesha usugu mkeo ni nini?au raha yako kwenye nyumba asijulikane nani mama au baba kwa kuvimba misuri???????

wababa wa aina hii jamani baada ya ndoa mkeo ndio kila kitu chako, sasa usipoweza kukitunza vyema shaurilo....

Reactions:

0 comments:

Post a Comment