Monday, October 4, 2010

MWANAMKE UTALIA NA NDOA YAKO MPAKA LINI?


dhumuni la blog hii ni kuelimishana mambo ya nyumbani, waume zetu, wake zetu lakini dhumuni kubwa ni kuelimisha mwanamke..
wanawake wengi sana wanalizwa kwenye ndoa zao na wame zao, kila siku lazima mwanamke mmoja atalia kwasababu ya mume wake, labda mume wake hatoi hela ya matumizi nyumbani, mume wake mlevi sana, mume wake ni muhuni sana, mume wake anampiga sana, mume wake katelekeza watoto na vitu vingi sana.
mimi kama mke nilikataa kulia juu ya mwanaume siku nyingi sana, sio kwamba hayajanikuta ya kunifanya nilie hapana, ila yalikuwa mengi mpaka yakanikomaza na kunifanya nipate kuyatatua kinamna yangu na kwa kweli imenisaidia sana nadhani mume wangu anatamani sana aone tena chozi langu lakini hatakaaa..
mwanamke lazima ujifunze kusimama imara, haya maisha tunaishi mara moja tu ukifa leo hutakaa tena kurudi duniani uwe na mumeo na watoto wako tutarudi kwa maisha mengine kama vitabu vyetu vya Dini vinavyo sema..kwahiyo acha kabisa kulia kwasababu ya mwanaume mliyekutana naye hapa duniani akiwa na meno yake kamili na wewe pia...
kama mume wako hakupi hela ya matumizi utakaa ufe na watoto wako? maana ukishaolewa ni jukumu la mumeo kukupa hela ya matumizi sasa kama hata kidogo cha kupika chapati na maandazi haachi utalia kila siku? ndugu yangu kuna watu wanapesa na hawana pa kuzipeleka kunawababa waliofiwa na wake zao kutwa kugawa hela kwa watoto wadogo akija mmoja anayetaka kukusaidia utaacha? pokea hela endelea na maisha(utakachoamua kuendelea zaidi ya kupokea hela hayo ni maamuzi yako)....
kama mume wako hakupi chakula cha usiku, utafanyaje utaishi tu na njaa zako kisa kumfurahisha mumeo? sasa kama hakupi yeye anafanyaje njaa yake chakula anakula wapi? ndoa inakaaje mwezi, wiki, miaka mwanaume hajakupa chakula cha usiku sielewi kabisa na wewe umekaa tu ufe na njaa yako kama yeye hawezi kukupa basi tafuta wa kukupa rudi endelea na maisha yako na mumeo kwani inaandikwa usoni umetoka kula?
na kwa wanaume mnaopiga wake zenu kwani kumpiga mwanamke ni suluhisho, wewe unampiga kwa ngumi wenzako chobingo mwanamke anapigwa na upande wa kanga ikimshika tu mwilini kinachofwata watu walaaa chakula cha usiku maana kanga imeamsha hisia sasa wewe ngumi ukimpiga mkeo kutwa anabaki anaugulia maumivu unadhani atakuwazia kukupa nyoooooooo..
mwanamke utabaki kulia, ukijipa moyo mumeo atabadilika, wakati wewe unalia kila siku mwenzako maisha anayoishi na wewe anayafurahia tena na kupata wa kumliwaza nje, akija ndani wewe ndio wakufanyiwa vurugu na kulizwa..
ndoa mnatakiwa muifurahie sasa kama uliye naye hakufurahisi unafanyaje? mimi nilishakataa kuishi kwa mawazo nataka hata nikifa kesho nijuwe niliishi duniani nikafurahia maisha yangu ya hapa kwahiyo asiloliweza kunipa yeye nitapata tu (popote)...
narudia tena huu ni mtazamo wangu, simaanishi kila mwanamke akafanya haya lakini ukiona yanakufaa karibu kwenye jahazi...

12 comments:

  1. yaaani aisee sijui nikupe zawadi gani shost umeongea vizuri sana tena mno i wish wanawake wote wangesoma hii, safi sanaaaaaaaaaaaaaa mi mwenyewe mpaka nilie kwa ajili ya mwanaume aisee sijui hata ni lini maaana nilillia huko zamani na nilikuwa sijazinduka ila kwa sasa hanipati ngooo maana hawa wanaume wana maudhi sana na wala hayaishi kwa hiyo usipokomaa utakuja kufa bure kwa stress na mawazo kibao. gud idea keep it up

    ReplyDelete
  2. mie naamini mungu hakupi kilema usichoweza himili, wanawake tunateseka sana kwa wanaume lakini theres always a way out kama da rose alivosema hapo juu,lakini kamwe mwanamke ukimuonyesha mwanaume what u r made off, muonyeshe hujali na unaweza, kama yeye haleti hela ya chakula anza kujishughulisha, hii inaweza isiwe rahisi, lakini ukiweka nia utaweza, kama ni watoto kila siku waweke ndio your first priority, na pendeza kwa saana, na kila saa kua mtu wa kutabasamu,hata huo upumbavu wake atakua anaufanya huko huko, lakini si mbele yako, life is too short jamani!!!
    tum tum

    ReplyDelete
  3. tum tum nawe unanipa raha jamani haya wanawake oyeeeeee

    ReplyDelete
  4. babu wanawake tuelimike ee, yeye si wa kwanza na wala sio wa mwisho wako waliokuanza na watao kuja kesho. yey akisema wanini kuna wengine wanasema watakupata lini, akikupotezea na wewe mpotezee mazima. wasitutoe machozi hawana lolote na sisi tunaweza.

    ReplyDelete
  5. Halooo. Kikubwa tafuta miela mwenyewe atafyata. Mfanye akutegemee uone kama atathubutu kutikisa kiberiti. Mi nshamwambia mume wangu nipe talaka yangu wacha anune. Si kwa kuwa ananipenda kihivyo bali kwa kuwa akiniacha tu ameumbuka mashosti maana mimi ndo namfanya aitwe handsome jinsi nnavyomtunza japo hiyo ni siri yetu watu hawajuhi am the boss in the house when it comes to money.

    ReplyDelete
  6. SHOST NAANDIKA KWA CAPS KUONESHA KUFURAHISHWA NA TOPIC HIYO.YANI LEO ASABUHI NILIKUWA NAENDESHA HUKU NALIA BARABARA ZIMA WAKATI NAELEKEA JOB.YANI NALIZWA NA MME WANGU BALAA ILA KUANZIA LEO HALIONI TENA CHOZI LANGU.MTU NAJIFANYA SITOKI NJE YA NDOA KUMBE JAMAA LINATOKA LIKIRUDI USIKU LIMELEWA LINAKUTUKANA USIKU KUCHA NA KUTOA KASHFA KIBAO YANI MAJILANI WANAJISIKILIZIA TU.LIKILALA LINAKOROMAA WEEEEEEEEE.
    MAMA SAM

    ReplyDelete
  7. telling the truth da rose,hii mada imenigusa...m experiencing the same problem lakini tatizo m soo easily broken by mens acts.
    kwangu mie nimejaribu sana kujishusha kwa mume wangu lkn nilichokuja kukugundua ni kwamba wanaume cku zote hawana shukrani ht kidogo..cjui wanataka kila kukicha walambwe ndo fahari kwao?
    wanasahau kua nac pia wanawake walitutoa makwetu na tena bila mkopo,inanishangaza sana kipindi mwanzo wa uhusiano mwanaume wanakua wapole sana,lkn matokeo yake hapo bdae wakiona wamemilika ndo chanzo cha maugomvi yasiyo na msingi uanzia hapo.
    na km ndo kupendwa uko mmmh sa kweli imekua kerooooo.m really feedup wit men.they dont know without they r incomplete totally.

    ReplyDelete
  8. wanawake juu sanaaa, and yes we can, let the only reason that make us shade tears is happiness and not stupid selfish men.
    tum tum

    ReplyDelete
  9. weweeeeeeee leo kama kuna ushauri tofauti juu ya wanawake umegonga mfupa mana wengine husema piga goti muombee sali sana what for why not him nae asali kwa ajili ya familia kuwa na amani na upendo??? hilo ulosema ndo nilifanyalo kimya kimya cmshirikishi rafiki wala jirani kwani nao ni wachonganishi hawakawii kurudisha udaku vzr kuwa na mtu akupendae na kukuheshimu na kujua wewe nawe uko na familia... weraweraaaaaaaa!! wanawake tunaweza machozi mwisho kwanini ulielie bana kaza msuli.

    ReplyDelete
  10. Jamani hii mada imenigusa sana mana yameshanikuta ktika ndoa yangu, mwanaume hashikiki kwa umalaya, pesa ndani haachi, unyumba hakuna hata zaidi ya wiki. sasa hapo kuna nini tena? tena shuti anataka umvalishe ili akapendezeshe wengine inahuuuuuuuu! nikaamua kuchapa lapa saivi nna maisha yangu tena nimetulia tuli nikihitaji huduma nna pumziko langu ra roho linanifikisha kunako. Wanaume wa cku hizi wanapenda umariooo

    Mama Nora

    ReplyDelete
  11. Nimefurahishwa sana na mada hii kwa kweli wanawake tuache kulialia hilo ndio linampa mwanaume kichwa na kuzidi kukufanya ulie watu tunaumizwa na ndoa zetu lakini ukigangamala mwanamme hawezi kukubabaisha hata kidogo

    Mama Abuu

    ReplyDelete