Friday, October 8, 2010

KUWENI MAKINI NA HAWA WASICHANA WA KAZI...

jamani wenzangu kuweni makini sana na hawa wasichana wa kazi mwenzenu yamenikuta, nimepata msichana wa kazi maana kama mnavyojuwa ni vigumu sana kupata msichana wa kazi, basi nikampata huyu dada kwanza tu alivyokuja siku ya kwanza jamani alinitisha yani sura yake haina nuru kabisa, halafu anatabia ya kulazimisha sana yani mpaka watu ninaoishi nao wanashangaa..
sasa pamoja na huyu dada ninaishi na mdogo wangu anayenisaidia mwanangu jana akaniambia dada nilikuwa natafuta mafuta ya kujipaka chumbani kwa bahati mbaya nikadondosha begi la dada zikadondoka hirizi tatu zimefungwa kama mzigo....
jamani nilichanganyikiwa ukiangalia nina mtoto na mwengine yupo njiani, nikampigia kwanza mume wangu akaniambia kabla hatujalala huyo dada awe ameondoka na mama yangu akaniambia hivyohivyo, sasa kabla ya kujionea mwenyewe hizo hirizi nikamtuma dada gengeni ili niweze kukagua begi lake cha kushangaza akaingia chumbani na kubadilisha nguo kitu ambacho kilinishangaza kwanini hupenda kubadilisha nguo kila akitoka nje na kuvaa ile nguo aliyokuja nayo, kwenda kuangalia begi lake sikuzikuta bali nilikuta shanga nyingi (kitu ambachi sishangai maana mimi mwenyewe huvaa nyingi pia) na hirizi sikuziona...
nikaongea na watu wazima wakaniambia atakuwa ameshajuwa unaweza kumchunguza ndio maana kila unapomtuma lazima akavae ile nguo moja na anazivaa na hizo pia na kwanini kila siku avae hiyo tu, na huyu dada hana mapenzi kabisa na mwanangu nimeamua kumrudisha kwao niishi kwa amani, mume wangu anasema asije akatuachia jini bure kwenye nyumba lituangaishe..
kwahiyo wenzangu hebu kabla hamjakubali kukaa nao kabisa kuweni na mtindo wa kuwachunguza wasije wakawa wamekuja na mengi zaidi ya wao kufanya kazi na ndio maana siku hizi kila mara tunasikia vituko vya wasichana wa kazi wameffanya mambo ya ajabu.

2 comments:

  1. eeeh polee my dia, mungu azidi kukulinda na mabaya yote. hii kwa kweli inaogopesha....mungu atulinde sote kwa kila baya humu majumbani kwetu.
    tumtum

    ReplyDelete
  2. Pole mpenzi,mimi ilishanitokea nilimkuta ana hirizi kubwa km fuko la rambo,nikamvizia ametoka nikaanza sachi begi lake,mwenzangu cha kwanza kukutatan nacho shanga 5 kubwa km za shingoni,kaniki na shanga za kiunoni karibia 200 na vidonge vya majira pakt 1,nilichanganyikiwa ukizingatia binti mwenyewe alikuwa na miaka 16 tu,aliporudi nikamuuliza ile kumuuliza tu akanipandishia mashetani ya ajabu,likitoka la kimasai linakuja la kigogo,mara subiani mara jini simba ili mradi vurugu ilikuwa jumamosi saa 4 asb basi majini yalitibuka kuanzia saa 4 mpaka saa 10 jioni mimi siju kusema na majini namtazama tu ila nilikuwa nimemtoa uani, baadae nikamuonea huruma maana alikuwa anajirusha anajipiga chini mpaka damu zinatoka,nikampigia cm Bibi yake akaniambia eti nimshike sikio huku nikimsemea maneno mwenzangu nikaogopa, nikaamua kumuita Mchungaji wa kanisa la jirani akamuombea ndio akatulia. alipotulia nikampa Diclopar akazikataa akasema yeye hasikii maumivu yeyote nikashangaa nikachoka mwili na roho basi aliporudi mume wangu jioni saa 1 nikamsimulia akaniambia huyu halali humu ndani atalala Guest asb kwao na ndio ilivyokuwa kesho yake alfajiri tukamsafirisha.
    Mdau Mtwara

    ReplyDelete