Tuesday, August 3, 2010

BEKI TATU...

hivi kwanini wasichana wa kazi huitwa beki tatu na inamaanisha nini, kunamtu anataka kujulishwa jamani kwa anayefahamu..

3 comments:

  1. Hili wanaweza kulijibu vizuri wachezaji mpira hasa wale wa uwanja wa ndani, kuna mmoja hapa nimemuuliza anasema hiyo haina tofauti na wale wanapenda mafiga matatu, na huyo binti wa watu kwa waroho wanamfanya figa la tatu, yaani mke wako wa ndoa hawara na huyo anakuwa akiba ya tatu...hiyo ni kwa waroho kasisitiza

    ReplyDelete
  2. mh inamaana ni msaidizi wa nyumbani ni mtu wa tatu ambaye mmemwamini na kumthamini anakuwepo nyumbani masaa yote na kama kuna tatizo au dharura atawajulisha that is

    ReplyDelete
  3. Maisha yanapangwa hivi! Katika umuhimu wa watu walionyumbani kwako utake usitake ni lazima umuhimu wa kwanza utampa mkeo au mumeo huyo atakuwa beki namba moja. hiyo ni katika kumpa kitu au kumueleza matatizo. Beki mbili ni watoto, hawa hawaelezwi kitu mpaka kwanza ameelezwa mama yao au baba yao. hata katika kununua kitu unamnunulia mume au mke ndio watoto ndio maana wanaitwa beki mbili. Baada ya hapo sasa kama kuna umuhimu wowote ule hapo ndipo tunamjulisha beki namba tatu yaani HouseGirl Huyu siku zote ni wa mwisho kujua kitu chochote. lakini ni mtu muhimu sana kwa kubaki na nyumba. Ndio mtazamo wangu......Kizito!!

    ReplyDelete