Tuesday, June 1, 2010

UTASA....

tunaamini na kujua ya kwamba sisi kama binadamu tunafanya tu lile tendo la ndoa ili mbegu zikakutane na yai kutengeneza mtoto, lakini tusisahau ya kwamba sisi tunatoa tu mbegu na yai lakini ni Mungu ndiye anayetengeneza mtoto..

nasikitika jamii sikuhizi ukichelewa tu kubeba mimba wanaanza kukusema ya kwamba wewe ni tasa, ama utakuwa umetoa mimba nyingi sana ndio maana sasa hivi hazikamati tena kisayansi hayo yote yanawezekana lakini je sayansi hiyo ni kubwa kuliko Mungu?

kwani nyie wawili si mara kibao manafanya tendo la ndoa ili kutengeneza mtoto sasa kwa nini mmoja awe tasa, kama ni hivyo basi wote wawili ni matasa.. ninachotaka kusema ni kwamba tusiwe na haraka ya kuhukumu mtu ya kwamba ni tasa labda bado Mungu hajampa muda wake wa kupata mtoto..

ushuhuda mkubwa niliyo nao ni baba yangu mdogo na mke wake wameoana na kukaa miaka kumi na nne bila mtoto lakini Mungu amewafanyia maajabu wakapata mtoto na sasa mtoto wao ana mwezi tangu azaliwe, wenyewe hawajaamini na mpaka sasa hawaamini mpaka imefikia hawawezi kulala usiku wanatumia muda wao mwingi kumshangaa mtoto wao..

jamani tusiamini kuhusu swala la utasa tumuombe Mungu na kumsubiria kwa wakati wake atupe mtoto....

0 comments:

Post a Comment