Friday, June 4, 2010

MAPISHI.......


chakula ndio mafuta ya maisha yetu ya kila siku, kwani hutupa nguvu ya kuweza kuishi na kujiletea maendeleo..
mapishi nyumbani ni muhimu ili familia ipate kuwa na afya, cha kushangaza ni kwamba kuna wake wengine swala la mapishi kwao limekuwa ni la ajabu, kwani nimesikia kaka mmoja akilalamika kwa rafiki zake kwamba mke wake hapendi kabisa kupika na tokea wameoana huu ni mwaka wa tisa sasa huyu mama hajawahi hata siku moja kumpikia, na kwavile hawana watoto wala msichana wa kazi huyu baba siku zote hizo alikuwa akila hotelini mpaka alipoamua kuwa na mwanamke nje (kidumu) wa kumpikia na kumpa mambo mengine ambayo mke wake anashindwa kumpatia..
jamani kina mama, tujitahisi hata kama tunakazi nyingi sana, tujipe japo hata siku moja ambayo tunakuwa tupo nyumbani tuwe tunawapikia familia zetu na haswa wame zetu haijalishi kabisa kama unacheo kikubwa kuliko mume wako ama kama unakazi na mume wako hana..
utakuta mama hata siku moja hajawahi kumpikia mume, siku zote anamuachia msichana wa kazi ampikie mumewe huu si utani sasa, utakuta dada wa kazi katoka zake kijijini ambapo hamna hata nyanya ni mwendo tu wa kuchemsha kila kitu kama nyama, samaki na venginevyo sasa unategemea mumeo atakula vya kuchemsha mpaka lini? maana yake raha ya kuwa na mke mume apate afya kwa kula kila aina ya mankodikodi, marosti, pilau, birihani, chapati na vyengine vingi sasa huyo dada wa kazi unayemuachia apike kama hawezi kuvipika hivi vitu inakuwaje??? hehehe ndio mwanzo wa familia yako kuonekana kama wanautapiamlo jamani...
wewe mama muonekano wa kiafya kwa familia yako ni jukumu lako basi tulifanye kwa usafi na upendo kwa manufaa ya familia zetu....

1 comments:

  1. asante kwa topic hii nzuri dada hili suala ni muhimu kweli, mimi ni mwanaume ambaye kutopikiwa kwangu imekuwa ni kawaida. kupikiwa, kutayarishiwa na house girl ni kitu cha kawaida,pia kila nirudipo kazini mke wangu huwa hayupo nyumbani anayenipokea ni msichana wa kazi mke wangu amekuwa bize kweli na mara kwa mara nimekuwa nikifanya ngono na msichana wa kazi pia nashukuru mke wangu hajawahi kugundua.Sipendi kufanya ninavyofanya lakini najistukia navutiwa naye ninafanya naye kitendo. Endeleeni kuelimisha labda wa mama watajirekebisha na kuamua kuwalinda waume zao.House girl hakatai hata siku moja siku ikitoke ninakula chakula ambacho nimeandaliwa na house girl nikahitaji maji ya kunywa, basi atamwambia dadaaaa embu mletee baba maji, basi ndo hivyo tumethubutu tunasonga mbele miaka nane ya ndoa.

    ReplyDelete