KUNA DADA MMOJA ALIPATA MCHUMBA, NA KATIKA UCHUMBA WAO KAMA UCHUMBA MWENGINE WALIPENDANA SANA NA KUAMINIANA SANA
NA KAMA MAHUSIANO MENGI AMBAYO TUMEPITIA AMA TUMEHADITHIWA AU PIA KUONA NI KIPINDI CHA MWANZO TU AMBAPO WAKATI WA MZUNGUKO MNAVAA CONDOM LAKINI SIKU ZINAVYOENDELEA MMESHA ZUNGUKA ZAIDI YA MARA TATU MNAANZA KUAMINIANA NA KUDANGANYANA NA KUACHA KUTUMIA CONDOM
HAIKUA TOFAUTI KATI YA JAMES NA RHODA, BAADA YA KUONA WAMESHALALA PAMOJA ZAIDI YA MARA TATU WAKAAMUA SASA KUANZA KU DU BILA KINGA, NA WALIFURAHIA KWELI MAANA RAHA ZILIZIDI ZAIDI YA MWANZO HUKU JAMES AKIMSIFIA RHODA KUWA NA UKE WENYE MAJI HACHUKUI MUDA KUANDALIWA NA MWANAUME ALIKUA AKIFURAHIA SANA HUO MTELEZO
RHODA NI KATI YA WANAWAKE AMBAO NILIWAFUNDISHA YA KWAMBA WAKATI WA KU DU TULIZA AKILI, TAMANI LILE TENDO, TAMANI ULE UUME WA MPENZI WAKO NA UJIACHIE MWILI UTASIKIA RAHA YA AJABU NA HAUTAKUA MKAVU MAANA ILI KUENJOY TUKIO AKILI LAZIMA IJUE INATAKA KUPOKEA NINI CHA RAHA GANI NA UTAMU UPI
RHODA MIAKA YA NYUMA ALISUMBULIWA SANA KATIKA MAHUSIANO YAKE NA MPENZI WAKE WA MWANZO KUFIKIA MPAKA AKASEMA HATAKAA APENDE TENA NA ILIMCHUKUA MUDA MPAKA KUJA KUMKUBALI JAMES, NI BAADA YA KUONGEA NAE SANA NA KUMSIHI AACHILIE MOYO KWANI SIO WANAUME WOTE NI WASHENZI KAMA YULE ALIYEKUA NAE MWANZO KWAHIYO KATIKA KILA STAGE AIPITIAYO RHODA AKITAKA USHAURI HUWA ANANIFWATA.
LAKINI KUHUSU JAMES ALINIFICHA MPAKA HAYA YALIPOMTOKEA NDIO AKAJA KUNIHADITHIA AKILIA NA KUWA NA MSHANGAO MWINGI..
BASI MAPENZI KATI YAO YAKAWA MOTOMOTO YANI KILA MTU ANAENJOY PENZI LA MWENZIYE, WAKITAKA MCHEZO UNAFANYIKA KATIKA UWANJA WOWOTE SASA SIO LAZIMA CHUMBANI KWAKUWA SI KILA MMOJA ALISHAMPA MWENZIYE MWILI WAKE..TUNDA LILE KAMILI BASI RAHA TUPU
KAFIKA SASA KIPINDI WALIPENDANA MPAKA JAMES AKAMUA KUPELEKA BARUA YA UCHUMBA KWA KINA RHODA AKITAKA KUMUOA RHODA
BARUA IKAPOKELEWA, PROCESS ZA HARUSI ZIKAFANYIKA SHOGA AKANILETEA KADI NIKACHANGA AKAOLEWA MWEZI WA KUMI MWAKA JANA, KWAKWELI HARUSI YAO ILIPENDEZA SANA SANA
MWEZI WA KWANZA SHOGA AKANIPIGIA SIMU DADA NINAHABARI NJEMA NATAKA NIFURAHIE NAWE NINAMIMBA!!!! KWAKWELI NILIFURAHI SANA NAKUMTAKIA KILA LAHERI KATIKA MIEZI TISA YA MIMBA MAANA SIO MIGUMU WALA SIO MIRAHISI BALI UNAHITAJI MKONO WA MUNGU ILI UVUKE SALAMA MPAKA KUPATA MTOTO WAKO
BASI SHOGA AKAKATA SIMU SIKUMSIKIA TENA MPAKA IJUMAA HII YA JUZI SINTOKAA KUSAHAU 25/4/2014 AKANIPIGIA SIMU HUKU ANALIA AKINIOMBA KUONANA NA MIMI ANAHITAJI KUONGEA NA MIMI BASI TUKAPANGA TUKAENDA KUONGEA KATIKA HOTEL FULANI MAANA MOYONI NILIJUA HUYU ANAHITAJI KULIA SANA SASA NIKIPANGA NAYE SEHEMU AMBAYO NI YA WAZI ITALETA BALAA
JUMAMOSI MCHANA NIKAENDA KWENYE HIYO HOTEL ALIKUJA, TUKASALIMIANA NIKAMKUMBATIA TUKAAGIZA VINYWAJI NA KUMUULIZA TU VIPI MAISHA IN GENERAL AKANIJIBU VIZURI TU
NIKAMUULIZA VIPI MUMEO HAJAMBO??? AKANIAMBIA MUME WANGU?????? MUME WANGU NDIO ALIYENIFANYA NIJE KUKUONA DADA NIKAMUULIZA KWANINI KWANI KUNA TATIZO MARA MACHOZI YAKAANZA KUMTOKA YAKATOKA MENGI KIASI KILA ALIKUA AKIJIFUTA YANAZIDI KUMWAGIKA NIKAONA NDANI YA MOYO WAKE ANAKITU KIMEMBANA ANAHITAJI KUKITOA
NILICHOMWAMBIA NI KWAMBA RHODA NAKURUHUSU ULIE LIA SANA MAMII HAPA HAKUNA ANAYETUANGALIA NIKAMKUMBATIA AKALIA SANA YANI ALILIA SANA ALILIA MNO SIKU ILE MPAKA KWIKWI LAKINI SIKUMYAMAZISHA NILIMKUMBATIA TU ALIE..MPAKA ALIPONYAMAZA NDIO NILIPOANZA KUONGEA NAE
NIKAMUULIZA TU SWALI MOJA..TATIZO NI NINI?? AKANIAMBIA DADA NILIPOMPATA JAMES SIKUPIMA NAYE AFYA NILIPOPATA HII MIMBA JAMES ALINIPELEKA CLINIC YANGU YA KWANZA NA TUKASHAURIWA KUPIMA AFYA ZETU WOTE WAWILI...ALIPOFIKA HAPA AKAANZA KULIA TENA
KWA AKILI YANGU NIKAJUA NA KUJIMALIZIA LABDA WAMEATHIRIKA, NDIO MAANA ANALIA SANA...AKANIAMBIA DADA MAJIBU YALIPOKUJA JAMES AKAKUTWA AMEATHIRIKA LAKINI MIMI NILIKUA MZIMA...
KWAKWELI MIMI MWENYEWE NILISHTUKA LAKINI KWA KAZI YANGU HII HUWEZI KUMUONYESHA MTEJA KWAMBA UMESHTUSHWA, NA WALA HUWEZI KUANZA KUHUKUMU WALA KUCHOKONOA MAMBO YA SIYOKUHUSU KWA ZAIDI WALA KUMLAUMU KWANINI HUKUPIMA WALA KUMSEMA KWAMBA ULITAKIWA UPIME KABLA YA KU DU NAE...SIO WAKATI WAKE SASA
NIKAMWAMBIA RHODA KWANZA HONGERA MPENZI YA KWAMBA WEWE NI MZIMA NA MUNGU AKIPENDA MWANAO ATAKUA MZIMA, NA POLE KUHUSU MUMEO. LAKINI BAADA YA KUGUNDUA MUMEO ANAHALI HII UMEFANYAJE MAMII
ANANIAMBIA NIMEANZA KUJIKUTA NAMTENGA, SINA TENA MAPENZI NAYE NAMUOGOPA, SIONI RAHA KULALA NAYE KITANDA KIMOJA WALA HATA KUWEKA MSWAKI WANGU PAMOJA NAYE NAHISI ANAWEZA TU AKANIFANYIA MAKUSUDI ANIAMBUKIZE NA MIMI
NIKAMWAMBIA HUPASWI KUFANYA HIVYO KAMA MKE HAPO NDIPO UNAPOTAKIWA KUSIMAMIA LILE AGANO LA KATIKA AFYA NA MAGONJWA ULILOLIAPA KANISANI LAZIMA KAMA MKE UMSAIDIE MUMEO KUPITIA HILI JANA ANAKUHITAJI WEWE ZAIDI, MAANA HATA YEYE UTAKUTA HAJUI KALITOA WAPI LAZIMA LITAKUWA KATIKA HAO WANAWAKE WAKE WA ZAMANI MAANA NDOA YENU NI MBICHI SANA AU LABDA KAMA ALIAMUA KUCHEPUKA LAKINI SITAKI KUAMINI KAMA ALIPATA MWANAMKE MPYA TU NA KUCHEPUKA ASILIMIA KUBWA NI KWAMBA ALIPATA KABLA YA NDOA.
NAJUA NDANI YA MOYO WA MUMEO ANAWAZA KATI YA WALE WANAWAKE FULANI ALIOKUA NAO NI NANI AMEMUAMBUKIZA LAKINI HAWEZI KUKWAMBIA, NA WALA HAWEZI KWENDA KUWAULIZA MAANA ATAZIDI DHARILIKA KWAHIYO MORE THAN EVER ANAKUHITAJI WEWE UWE BEGA LAKE LA KUEGEMEA WAKATI HUU MGUMU KWAKE
AKANIAMBIA SASA DADA NIFANYAJE, NITAWEZA KWELI??? NIKAMWAMBIA UTAWEZA KWANZA KABISA KUBALIANA NA MOYO WAKO KWAMBA MUMEO ANAUMWA NA ANAKUHITAJI, KUBALIANA NA MOYO WAKO KWAMBA MUMEO ANAHITAJI ASIWE NA MAWAZO NA KULA VIZURI PAMOJA NA KUTUMIA DAWA ILI AZIDI KUWA KATIKA MAISHA YAKO NA MTOTO, NIKAMWAMBIA NI BORA BABA AWEPO TU HATA KAMA MLEMAVU KATIKA MAISHA YENU KULIKO ASIWEPO UTAPATA TABU SANA NA MTOTO, NA UJUE MTOTO ANAHAKI YA MAPENZI YAKO NA BABA YAKE
AKANIAMBIA KWELI DADA NITASIKITIKA SANA KAMA MTOTO WANGU ATAKUA BILA BABA, NA NITASIKITIKA SANA MUME WANGU AKIFA KISA SIJAMTUNZA YANI KWELI NIWE MJANE NA UDOGO WOTE HUU...AKAANZA KULIA NIKAMWAMBIA UDOGO GANI ULIOKUWA NAO UKISHAJUA KUKATIKA KIUNO KITANDANI, UKAPATA MUME NA KUBEBA MIMBA UJUWE WEWE SIO MDOGO TENA YANI UMEKUA NA UKISHAKUA MKUBWA UKUBALIANE NA CHANGAMOTO ZOTE ZA MAISHA SASA FUTA HIYO KAULI YAKO YA UDOGO NA USEME WEWE NI MKE JASIRI, NA MAMA WA SHOKA..AKACHEKA NA KUSEMA HIVYO
TUKALA, NIKABADILISHA TOPIC ILA NIKAENDELEA KUPIGA STORY NYENGINE YA JINSI ILIVYORAHA NA KUWA NA MUME, NA MAPENZI NDANI YA NDOA KWA UJUMLA ILI KUZIDI KUMJENGA AWEZE KUMPENDA TENA MUMEWE, TUKAONGEA SANA BAADAE TUKAACHANA KILA MTU KUREJEA MAKWAO LAKINI ALIONDOKA NA MOYO MWEUPE, MWENYE UCHU WA KUTAKA KUMPENDA SANA MUMEWE KWA HIKI KIPINDI WALICHOBAKIZA NA KUTAKA KUJENGA FAMILIA BORA..AKANIAMBIA ATAKUA SANA MAKINI KATIKA KUMPA LISHE BORA MUMEWE NA KUMPA DAWA ZAKE KWA WAKATI..NA KATIKA KU DU KASEMA WATATUMIA CONDOMS TU ANAOGOPA ANAHISI ATAAMBUKIZWA SIKU, BORA AJIHAMI.
*****END******
Tuesday, June 17, 2014
mmmmhh ni ngumu sana kumeza....
11:02 PM
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment