Kuna wachumba walipendana mnooo na walikuwa waaminifu wakati wa uchumba wao. Waliahidiana kutokufanya tendo la ndoa hadi siku ya ndoa. Mwanamke akamwambia mchumba wake kwamba hajawahi kushiriki tendo hilo na yeye (mkaka) ndo atakuwa wa kwanza. Waliishi ktk uchumba kwa miaka 2 na wakafunga ndoa.
SIKU YA NDOA: Wazazi wa pande zote walisafiri toka mbali tena vijijini huko na ndoa ilifungwa jijini. Na aliitwa mchungaji maalum toka mbali kufungisha ndoa hiyo:
ASALI YA MWEZINI (HONEYMOON): Jamaa akakuta tofauti na alivyotarajia, asubuhi kamwacha mkewe Hotelini, akaenda kuwaambia wazazi wake kwamba amesalitiwa na mkewe maana JOGOO WAMEDONOA MCHELE hivyo akasema kwa kuwa aliahidiwa angekuta SEALED na imekuwa kinyume chake basi HAMTAKI TENA. Mama wa Bw. Harusi pressure juu, Baba, mawifi, shangazi ndo usiseme. Jamaa akaenda kwa mchungaji aliyefungisha ndoa na kumueleza mkasa mzima. Mchungaji akamsikitikia kweli, akampa pole nyingi kisha akamuuliza:
1. Wewe ni mwaminifu? Jibu (ndiyo),
2. Umejuaje kwamba JOGOO WAKIDONOA MCHELE kunakuwa na hali fulani na WASIPODONOA kunakuwa hivi? (Kimya)
3. HUJAWAHI KUDONOA MICHELE YA WENGINE? (Machozi, kutubu na kumkimbilia mkewe Hotelini na kumuomba msamaha).
FUNDISHO: Usimuhukumu mwenzio kwa dhambi au kosa ambalo nawe ulitenda.
No comments:
Post a Comment