Monday, May 26, 2014

Leo nina story ya mtu na baba mtoto wake...

Basi bwana kuna dada mmoja anaishi na mpenzi wake wakabahatika kupata mtoto mmoja wa kike

wamekuwa wakiishi kwa muda mrefu, japo wazazi wa mwanaume hawakumpenda yule mwanamke, na walikuwa kila mara wanamshauri mtoto wao kutafuta mwanamke mwengine wa kumuoa lakini sio huyo mama mtoto wake

na bila sababu mama mkwe alitokea tu kumchukia yule dada wa watu, msichana sio mcharuko useme labda anamsumbua kaka wa watu hapana maana hata mimi kuna kipindi nilishawahi kuishi naye miezi miwili kwahiyo ni msichana ninayemfahamu

huyu dada yeye kwao ni morogoro na huyu mwanaume ni muarabu wa kipemba kwahiyo labda makabila yao ndio yalikuwa yanaleta matatizo kwenye mahusiano yao maana nyumbani kulikuwa hamna amani yani ipite mwezi hawajagombana kisa mama mkwe hamtaki haijawahi tokea

muda ukaenda sasa sijui kwasababu ya maneno ya mama yake kwamba hamtaki yule msichana huyu kaka akapata mwanamke mwengine nje (hawara) mtoto wa tanga akaanza naye mapenzi

basi bwana tena mapenzi motomoto kwa mtoto wa tanga, japo pia mama yake hakumpenda huyu pia lakini mwanaume tena ndio kashapenda na hivi dini yake inaruhusu alikuwa hajionei hata akiamua kuoa wote wawili kwa wakati mmoja

mbaya zaidi kilichokuwa kinasikitisha yule kaka alianza kubadilika nyumbani kwake harudi, ahudumii mtoto wake, yani akawa mkali sana

mbaya zaidi alimpa uhuru sana mwanamke wake wa nje mpaka kumdharau mama mtoto wake maana huyu dada anasema ikaanza yule hawara anampigia simu na kumtukana sana, na kumwambia yeye ndiye atakayeolewa kwamba shoga unapoteza tu muda ondoka huyo mwanao nitamlea 

wakawa wanatukanana sana wakitukanana huyo hawara anamueleza bwana ake akirudi basi yule bwana akirudi nyumbani anakuwa kama mbogo anagombana sana na mama mtoto wake mpaka kumpiga sana

maisha yakawa yanaendelea hivyo mapenzi tena hakuna amani yameshaingiliwa na kidudu mtu, basi huyu mama mtoto akawa anajitahidi sana kutopokea simu za yule dada maana aliamua kusave number yake yule hawara akabadilisha number akimpigia akipokea tu matusi sanaaa

cha kushangaza huyo hawara anamchamba mpaka mama mkwe kwamba unmwambia mwanao aoe mpemba mwenziye yani asiponioa mimi huyu labda sio mtanga mnajua ninachompa!!!!!!!! mama mkwe hoi kapata kiboko yake

hawara kachachamaa mama mtoto afukuzwe, na kweli yule mwanaume juzi katoka kazini kamfukuza mama mtoto wake na mwanae...

mama mkwe kusikia sasa anatapatapa na huyu mama mtoto kumuomba msamaha kwamba afanye juu chini ahakikishe anarudiana na mwanae, yani simu kwa sana akimbembeleza huyu dada

itakuwaje baadae nitawajuza...****END*****

No comments:

Post a Comment