Friday, May 23, 2014

Leo nataka kuongelea ukomavu wa mwanamke katika ndoa...

katika maisha ya ndoa kama sio kusikia basi tumeona ama wenyewe inatutokea kwamba wanawake ndio wenye kubeba familia, kila kinachotokea kwenye ndoa kiwe kibaya ama kizuri mwanamke ndiye anayetakiwa kukabiliana nalo bila kupinga

ifike sehemu kwenye ndoa zetu wanawake tuishi kwa amani, upendo wa kweli na kutaka kweli kuwa kwenye hiyo ndoa sio tu kwasababu ya uvumilivu uliofundishwa kwenye kitchen party basi ukavumilie hata yasiyovumilika

ama uoga wa kuonekana umeachika na marafiki zako au ndugu au kuwazia ile harusi ya ghali sana mliofanya na hekaheka zote za kitchen party na sendoff zikakufunga wewe kwenye ndoa isiyoweza kurekebishika

 leo nimeumia sana kuamka asubuhi na kupata taarifa kwamba mke wa shemeji yangu alikunywa vidonge ajiuwe kisa wamegombana na mumewe

magombano kwenye ndoa ni mengi wanaume wanatupiga, wanatutukania wazazi, wanalala nje kisa kagombana na mkewe, yote hayo ya kuumiza moyo tunakutana nayo kwenye ndoa lakini je wewe kama mke unapokeaje matatizo yako ya ndoa

ukinywa vidonge ama sumu ufe je utakuwa umetatua lile tatizo?? watoto wako unamuachia nani mwanaume yeye hatajali umekufa wewe ndani ya miezi mitatu kaleta mwanamke mwengine ndani shoga tena umkute ndugu yake shetani watoto wako watateswa sana

maisha ni zaidi ya kuwa na mume kwamba useme mimi baada ya kuolewa sasa maisha yangu ndio yamesimama kila anachotaka mume wangu nifanye, HAPANA

ndoa ni mpango wa MUNGU wala hakuweka ndoa kuwa adhabu bali alitaka tupendane kwa dhati, tuheshimiane,kila mtu amjali mwenziye, tuzae watoto tuwalee vyema kwenye maadili mema na ya kumpendeza MUNGU na basi utakapoamua kuoa fulani ama kuolewa na fulani ni kifo tu kiwatenganishe sio umalaya, sio ulevi,sio hasira,sio kupigwa bali KIFO tu

lakini unapoona kabisa ndoa yangu hii tumejaribu sana kuilea, tumekalishwa sana vikao na wakubwa na wasimamizi wa ndoa lakini bado hakuna mabadiliko labda ni muda wa wewe kukaa pembeni na kuanza maisha yako upya kama unawatoto lea wanao anza upya

sio kwamba ukichana na mumeo hutakula, hutavaa au wanao wanatishindwa kwenda shule na kuwa na maisha mazuri hapana..

muda ukifika kubali kuolewa unapoingia kwenye ndoa nenda na moyo wa ukomavu na ujasiri, tumikia vyema ndoa yako, lea vyema watoto wako na mumeo, jiendeleze kifedha na kimasomo, usikubali kukaa na kuwaza ama kujutia kwanini uliingia kwenye ndoa inayokupa mateso

bali changamoto zako za ndoa zikujenge kuwa mwanamke hodari, mwanamke imara, mama wa mfano kesho watoto wako na watu wengine wakuheshimu kwakuwa mwanamke shujaaa

******END******

No comments:

Post a Comment