Tulopotosheka tukiwa tumelala kitandani kila mmoja wetu akitafakari tukio lililoisha tulikaa kimya dakika kama kumi huku tumekumbatiana bila mtu yoyote kuongea kitu
Ghafla nikasikia mkono umepita juu ya tumbo langu huku akinipapasa kwa huba akaniambia itakuwaje baada ya hapa,najua hutoruhusiwa tena kutoka na ukirudi utakuwa ugomvi kwakuwa ulimtotoka dereva
Nilikaa kimya nikitafakari cha kumjibu nikajikuta sina la kuongea..tukajiandaa nusu saa baadae na kuondoka kabla sijafungua mlango wa hotel alinivuta mkono akanisogeza karibu yake mikono yake ikiwa inanipapasa shingoni na kwenye nywele zangu akanibusu kwa mahaba na kuniambia ananipenda..nikaondoka
Nikiwa njiani kurudi nyumbani nikawasha simu na kupokea msg kutoka kwa mume wangu dereva amempigia kumwambia sikuwa nyumbani alivyorudi kariakoo nimpigie nitakapowasha simu
Nikampigia na kumwambia mume wangu mgonjwa alihitaji maji ya madafu kwahiyo nikakimba ufukweni coco kumnunulia..mume wangu alinifokea sana na kuniambia hiyo sio kazi yangu ningemtuma dereva atakaporudi niliomba msamaha mume wangu akanikatia simu
Nikamkuta dereva nyumbani akanichukua kunirudisha nyumbani goba, Maisha yakaendelea huku nikiwasiliana na mpenzi kwenye simu tu kama miezi mitano mfululizo tuliumia sana kushindwa kuonana lakini hatukuwa na la kufanya
Mwezi wa sita wake mdogo wangu akatambulisha mchumba nyumbani wakaamua kumfanyia sherehe ndipo nikamuomba mdogo wangu amualike na mpenzi wangu nilikuwa na hamu hiyo jumapili ifike nikamuone mpenzi wa roho yangu
Jumapili ilipofika tukaenda nyumbani kwa ajili ya sherehe baadae mpenzi alikuja kwa jinsi alivyopendeza na nilivyomkumbuka nilitamani kumrukia na kuanza kumbusu..lakini sikuweza tuliishia kuangaliana kila mtu akimtamani mwenziye
Tulijitahidi kuficha hisia zetu sherehe ikaisha kila mtu akaondoka tukarudi nyumbani, Kutokana na mapenzi kunizidia nje sikujua ndani niliyapunguza mume wangu akaanza kunichunguza kwanzia na simu yangu
Anasema alienda kampuni ya simu na kuangalia niliyoyafanya kwenye simu yangu na kugundua hiyo number inayonipigia mara kwa mara na muda huohuo
Bila mimi kujua mume wangu anafanyaje siku akaniaga anasafiri mimi nilifurahi nikijuwa nimepata wiki nzima ya kuweza kumuona mpenzi nitakapo..mume wangu akaondoka
Mimi siku hiyohiyo nikampigia mpenzi na kwenda nikakaa huko tukifurahia penzi jioni nikarudi nyumbani
Siku ya pili na ya tatu pia hivyo hivyo tulikuwa tunajiachia tukijua tuko peke yetu tunafurahi
Kumbe wakati wote huo mume wangu alinifwatilia nyuma na kujua nyendo zangu siku ya nne nikiwa nimeenda kukutana na mpenzi ile tumemaliza tunataka kuondoka gari ya mume wangu ilisimama mbele yetu ikatukinga na kushindwa kuondoka
MUNGU wangu mume wangu!!!!!! tulibaki tukiangaliana mume wangu akafungua mlango wa dereva bila mafanikio kwakuwa ulikuwa umelokiwa akavunja kioo na kufungua akamtoa mpenzi wangu na kumpiga sana alimpiga sana mpaka damu zikaanza kumtoka puani na mdomoni mpaka alipokua amelala hawezi hata kujitetea mume wangu akanivuta mkono kuniingiza kwenye gari yake tukaondoka na kumuacha mpenzi wangu pale
Mume wangu alikimbiza sana gari huku akihema sana nikajua tutagonga tushindwe kufika nyumbani. Tulipofika nyumbani akanivuya kutok kwenye gari akaniwash vibao viwili vya nguvu sana na kuniacha hapo akaingia ndani
Nikaingia ndani cha kwanza nikaenda bafuni kuoga nilikuwa nalisa sana uchungu mara mbili wa kupigwa na kumuwaza mpenzi wangu sijui huko alipo anahali gani sijui watu walimuokoa
Sikuweza kumpigia simu nisije kusikia nikauliwa basi nilisali tu na kwenda kulala
Kesho yake asubuhi mida ya saa mbili napigiwa simu ma mtu anasema alimokota mwanaume akiwa na hali mbaya sana na wakamkimbiza hospital lakini kabla hajafika hospital alifariki
..tumeamua kupiga simu number zilizokwenye simu yake ili ndugu zake wamfwate hapa muhimbili mtatukuta
Kesho yake asubuhi mida ya saa mbili napigiwa simu ma mtu anasema alimokota mwanaume akiwa na hali mbaya sana na wakamkimbiza hospital lakini kabla hajafika hospital alifariki
..tumeamua kupiga simu number zilizokwenye simu yake ili ndugu zake wamfwate hapa muhimbili mtatukuta
Nilisikia kama nimemwagiwa maji ya baridi nilipiga mayowe na kulia sana nilishindwa kuvumilia..na jana ndio ilikuwa siku ya mwisho kumuona mpenzi wangu
Siwezi hata kumwambia mume wangu.....sidhani kama nitaweza kupenda tena kama nilivyompenda mpenzi wangu...na ninajipanga kuachana na mume wangu maana siwezi kuishi na mtu aliyeniondolea furaha ya pekee kwangu ukiacha mtoto wangu...
*****END*****
No comments:
Post a Comment