kuna kaka mmoja shekh ameoa na anawatoto wawili, wanaishi vizuri tu na familia yake..
kama tunavyojuwa hizi dini zetu tunaruhusiwa kuoa mke wa pili ila kwa kukubaliana tu na mkeo wa kwanza na unaweza kufanya hivyo mpaka wake wanne
basi huyu kaka akawa amempenda mdada mmoja na kumuomba mkewe kama angeoa mke wa pili, kwa mapenzi ya mkewe wala hakuwa na gubu bali alimkubalia mumewe kuoa mke mwengine
bwana akapata mwanamke kweli kama tunavyojuwa mapenzi yanavyokuwaga motomoto mnapokutana, basi yakaenda hivyo miezi kama sita wakaanza process za ndoa
wanaume wakajipanga kwenda kutoa mahari kwa mwanamke, walipofika kwa mwanamke mbwembwe zao zote za kuoa naona zilifika mwisho maana walipewa masharti magumu sana
wakwe wakamwambia bwana harusi kwamba mtoto wao hali maharage, hali mlenda hali bamia..yeye anakula nyama,kuku,maini tu
dduuhhhh kusikia hivyo ndugu wa mwanaume wakaanza kunong'ona chini kwa chini lakini kwakuwa jamaa alikuwa ameshampenda binti akakubali na kutoa mahari ndoa ilikuwa imepangwa mwezi ujao Tanga
basi karibia na siku ya ndoa shoga akasafiri kwenda Tanga kusubiri kuolewa pamoja na ndugu zake na mashoga zake
kama mnavyojua shamrashamra za ndoa mara uchorwe piko ukae ndani usingwe na vitu vyoote kama hivyo basi haikuwa tofauti kwa huyu shoga
upande wa pili ndugu wa mume walikaa na kijana wao chini na kumshauri je siunajua ndoa za kiislamu ukioa lazima nyumba zote mbili uhudumie sawa kwa sawa
na kwakuwa huyu shekh yeye alikuwa na nyumba aliyopewa ya urithi walitaka wake zake wote wawili akae nao katika nyumba hiyo watenganishwe na vyumba tu
sasa ndugu zake wakamwambia unadhani itakuwa vizuri mke mdogo akipika kuku wakati mke mkubwa kabandika maharage na wote wapo nyumba moja huoni kama unajitia dhambi na kumnyanyasa mmoja
basi wakamsemaaaaa wee yule bwana mpaka akili ikamkaa sawa
siku ya ndoa ikafika mwanaume akasema haendi kuoa kwamba masharti yamemzidia kule shoga yupo mwenyewe anajipamba anajua anakuja kuolewa
subiri subiri na yeye waapi siku ikapita,wiki na hata mwezi ikabidi sasa arudi dar ili ajue kwanini ameachwa kwenye mataa
ndio bwana na ndugu zake kuwaambia wakwe wameshindwa na masharti, kwani yeye alitaka kuoa mke ambaye watakuwa wote kwenye maisha ya shida na raha lakini naona huyu hayupo tayari na sitaweza kummudu
wakaomba kurudishiwa mahari yao, na wakapewa baada ya siku mbili na ndio mapenzi yao yakaishia hapo
shoga yupo tu mtaani na mapiko yake anazunguka watu wanamnyali tu..wenyewe wanamuita mama kuku
******END*******
0 comments:
Post a Comment