Tuesday, January 7, 2014

Kuoa na kuolewa ni bahati au ni Baraka... Part 3

akaniambia pumbavu kabisa wewe unataka kutuletea laana ya umasikini katika familia, yani umekosa mwanaume wa maana huko kazini kwenu ukatuletea huyo konda labda nife ndio atakuoa

nakwambia na baba yako akijua atakuua wewe unatuletea balaa 

nikamwambia mama watakuja kunioa na nitaolewa taka usitake mimi ndiye niliyempenda akanipiga sana akaondoka kwa hasira

baba aliporudi jioni akamwambia kila kitu baba akanifwata na kuniambia nataka uachane na huyo kijana la sivyo hutapenda matokeo yake

nikamwmabia baba siwezi kumuacha nampenda kwanini hamumtaki kwani umasikini aliupenda yeye hata yeye alijikuta tu humo kwenye hiyo familia nampenda baba nataka anioe

baba akaa kimya..ikapita mwezi baba akaniambia nimlete huyo kaka ajekuwaona, nilifurahi sana nikajua wamenikubalia maana wlaipika chakula nyumbani kweli konda akaja

hawakuonyesha kukasirishwa wala nini tukala tukanywa akaongea nao vizuri tu mara tukasikia hodi wakaingia wanaume wawili ndani baba akawaamuru wamchukue konda anamuharibia mtoto wake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

nililia kwa nguvu na kwa uchungu sana niliwakatalia lakini walinishinda nguvu na kumchukua mpenzi wangu akashtakiwa kwa kosa gani sijui na kufungwa segerea amini msiamini..alikaa jela miaka miwili

sikuchoka kwenda kumtembelea kila jumapili nilienda nilinunua chakula nikampelekea chakula cha break point kumkumbusha tulipokuwa tunakula tulipokuwa wote

bado akiwa jela aliendelea kunipenda nami nilionyesha msimamo wangu kumpenda yeye tu wazazi wangu walichanganyikiwa kwanini bado nilikuwa naye

baada ya miaka miwili baba aliomba kesi ifutwe na konda akaachiliwa huru, akarudi kwao hana kazi nikawa nawahudumia mpaka aliporejea hali yake ya kawasida

baba aliniomba msamaha kwa kufanya vile na kuamini kweli tulipendana alimuita konda na kumuomba msamaha na kuahidi kumsomesha baada ya kuoana

tukafanyiwa harusi kubwa sana na baba tukaoana na akatupa nyumba tabata ambapo tunaishi mpaka sasa

konda amepelekwa chuo yupo mwaka wa pili sasa anasomea finance chuo cha UD na MUNGU ametujalia tunamtoto wa kike sasa anaitwa anabel

*******END******

0 comments:

Post a Comment