kuna mama mmoja anaishi na mumewe na watoto wake wanne wa mwisho anamiaka miwili.
basi bwana yani huyu mama jamani utamueleza nini mumewe kwa mkewe, yani anampenda mkewe mapenzi ya ajabu kila kitu mkewe anachotaka afanye jamaa anafanya, mwanaume anafua, mwanaume anapika, mwanaume hata mtoto wao akimsema mama yao vibaya kama hujapigwa basi unafukuzwa nyumba
yule baba alikuwa hana marafiki, hana overtime kazini, hana majirani yeye na nyumbani kwake, nyumbani kwake na mkewe yani hata watoto walikuwa hawapati mapenzi anayompa mkewe..
Kwakweli wanawake wote mtaani tulipenda sana yale maisha anavyoishi na mumewe mpaka na sisi tukatamani tungekuwa nayo, basi mumeo akichelewa kurudi ama asipokusaidia kitu unaanza kulalama yani wanaume wengine sijui wakoje mbona mume wa fulani anampenda sana mkewe anamfanyia hivi na vile lakini wewe hata huwezi kunisaidia au kunifanyia
basi huyu mama mtoto wake wa mwisho walikuwa na urafiki mkubwa sana na mama wa jirani ambaye na yeye anamtoto waliolingana umri
huyu mama akawa amempeleka mwanaye shule hizi academy za mtaani sijui nyie kwenu pia mnazo maana kuna academy zinazojulikana kitaifa kama Green Acres, St Mary's, DIS,IST na nyengine nyingi lakini pia kuna academy za mtaani kama Juhudi English Medium, Mariam academy na nyengine ambazo ada zao ni 15,000-20,000 kwa mwezi
basi huyu mama akamfwata yule mama wa jirani na kumshauri kwakuwa watoto wetu ni marafiki sana kwanini usimpeleke na wewe mwanao kwenye ile shole anayosoma mwanangu ili wawe wote naamini watasoma wote tu vizuri kwakuwa wanajuana tokea nyumbani
basi yule mama wa jirani akamwabia ngoja nionge na mume wangu akikubali basi tutampeleka wawe wote..kweli yule mama akaongea na mumewe mumewe akakubali wakampeleka mtoto wao kwenye hiyo shule anayosoma mtoto wa bimkubwa
kweli huyu mama akamueleza mumewe na mumewe hakuona ubaya wakajipanga ndani ya wiki moja wakampeleka mtoto wao shule pamoja na mtoto wa bimkubwa
HAPA NDIO KASHESEH LILIPOANZIA...
kufika kule shuleni huyu mtoto wa jirani akawa anafanya vizuri sana yani mpaka mwalimu akawa anamsifia mpaka mwalimu siku hiyo akaja nyumbani kwa huyu mama kumsifia kuhusu mtoto wake
kwa bahati mbaya wakati mwalimu anaondoka njiani akakutana na bimkubwa wakaanza kusalimiana bi mkubwa akamwambia vipi leo upo mtaani kwetu yule mwalimu akamwambia nimekuja kuonana na mama James nimpe hongera ya mwanaye kwakweli yule mtoto anaakili na anafanya vizuri sana kuliko wenzake
looooohhhh mwalimu asijue alitangaza vita...
jamani amini msiamini yule mtoto ndani ya siku tatu alipatwa na homa kali sana, akawa hataki kula chochote yeye anataka mama yake tu ambebe wamehangaika hospitali zote hakuna ugonjwa unaoonekana yeye anataka kubebwa tu yani mama yake jamani amehangaika naye huyu mtoto hakuna maneno ninayoweza kuandika hapa yakabeba huo uzito ila naamini MUNGU BABA atawapa uwezo wa kusikia machungu ya huyu mama na mwanae
mtoto akakonda saaaana na cha kushangaza akaanza kuvimba tumbo yani ukimuona utasema anautapiamlo akaanza kupauka, yani alipatwa na kitu cha ajabu
shule tena ndio hamna akarudi nyuma kimasomo mama yake kila siku anasali na kuomba miujiza mwanaye apone, wapo waliomshauri kwenda kwa waganga lakini kwakuwa alikuwa anamtumainia MUNGU aliye juu alikataa kabisa akasema kama MUNGU anamtaka mwanaye basi amchukuwe lakini yeye ataendelea kumuombea na kuamini siku MUNGU atatenda miujiza
siku zilivyoendelea kwenda kila siku mtu unaamka unasikilizia yule mtoto sijui anaendeleaje, sijui mzima ama ndio kashaenda kupumzika maana jamani alikuwa anapata tabu sana
basi bwana kwakweli kila amtegemeae MUNGU hatamuacha aanguke kwenye mikono ya wabaya wake, siku moja akaja msicha wa kazi wa yule bi mkubwa nyumbani kwa mama wa jirani akaenda kuongea na yule mama kwamba mama naomba ninachotaka kukueleza usiende kumwambia mama atakuja kuniua
yule mama wa jirani anasema moyo ukanipasuka akaanza kumuuliza nini... ndio kuanza kuelezea kwamba hali hiyo ya mtoto aliyemsababishia kuwa hivyo ni bimkubwa
kwamba bi mkubwa siku alimtuma huyu msichana wake wa kazi akampa nyama akamwambia hakikisha hii nyama anakula mtoto wa jirani yule akija kucheza nyumbani kwetu, kweli kwakuwa alikuwa anaogopa kuduriwa yule mtoto alivyokuja kucheza kwao kama kawaida yake yule dada alimpa yule mtoto ile nyama akala ndio maana akadhurika vile
jamani yule mama alilia machozi, yule msichana wa kazi naye alilia huku akimuomba yule mama amsamehe kwa tendo alilofanya kwani naye anaumia kila siku anapomuona yule mtoto anavyopata tabu..yule mama baada ya kulia sana na kusali sana alimsamehe yule msichana wa kazi
lakini msichana wa kazi akamwabia si hayo tu bali yule mama ndani kwake anakibuyu huwa akitaka kitu chochote anaongelea kwenye hicho kibuyu na kinafanyika huwa namsikia anataja jina lako na la mwanao kwenye hicho kibuyu lakini sisikiagi huwa anasema mfanyaje
hata mumewe pia alishamuweka kwenye hicho kibuyu ndio maana unamuona mumewe zezeta sana ikija kwa mkwewe..bimkubwa ameshamchezea sana mumewe na sasa anampango wa kumuachisha kazi awe anakaa tu ndani asitoke nje
eeeeheeee lakini nakuomba amama usimwambie yule mama ataniua mimi, yule mama akaahidi kutomwambia yule mama ila alichofanya ni kesho yake kwenda kwa mchungaji kumchukuwa yule dada na mwanaye mchungaji kuingia ndani na kupiga sana maombi walikuja wachungaji watatu walisali sana sana siku tatu mfululizo
kwa miujiza ya MUNGU kila mtu mtaani aliiona yule mtoto alipona tumbo limeisha afya imerudi na jumatatu juzi ameanza shule mpya ile nyengine ameamishwa sasa maneno yanazunguka tu mtaani naamini siku yatamfikia yule mama maana anamuona sasa mtoto wa watu anaafya naamini anaona aibu na kujiuliza maswali mwengi..bila kujua hakuna linalomshinda MUNGU wetu
******END*****
Sunday, November 17, 2013
Usichezee uswahilini kwa uchawi yani kuloga kwao kitu kidogo sana wanajua waganga kama wanavyojuwa kuchagua madera kila shughuli dera jipya...haloooo
10:44 PM
1 comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mungu ni dawa tosha na ni mwaminifu. Uganga zake siku tatu tu Ila Mungu milele daima
ReplyDelete