Tuesday, November 26, 2013

Kila mwanamke ana jumamosi na ijumaa yake, hata wakikubania vipi ipo siku wataachia... PART 1

kama tunavyojuwa kuna kipindi tukifikaga tunaanza kuwaza na kutamani kwamba siku moja na sisi tuje kuolewa unaanza kupata picha sendoff na kitchen party yangu nataka iwe hivi na vile, nguo iweje rangi na kadhalika

 halafu katika wale wanaume ulionao kama ni watano au wawili unaanza sasa kuwapima nani anafaa kuwa mume au yule mmoja uliyenaye unaanza kumpatia picha siku akikuoa itakuwaje na mambo kama hayo

 ndivyo ilivyokuwa kwa dada mmoja anaitwa Neema na yeye alitamani hivyohivyo akawa anapenda sana kumuhadithia ndugu yake mmoja anaitwa Astazia kwamba siku yangu ya ndoa nataka iwe hivi na vile

 na kweli MUNGU alimbariki Neema akapata mwanaume mmoja wa maana anakazi yake nzuri sana alikuwa ni daktari anapesa yani alikuwa anajua sana kumuhudumia Neema wakati mwengine za weekend Neema alipenda kutoka na Astazia kwakuwa walikuwa wanaishi wote waende kuenjoy pamoja na huyu mwanaume wake Neema.

  mwanaume yule alikuwa anawapa raha sana wakina Neema yani kila mtu alikuwa anasema mwanaume si ndio huyu na kwakweli kwa mapenzi alimpenda sana Neema. mpaka Neema hakuamini kama kweli kuna wanaume wa aina hiyo hapa dar na kuwahadithia wenziye wa kazini na kufurahi nao..Neema yeye alikuwa anafanya kazi katika kampuni fulani ya magazeti alikuwa anaandika kuhusu mada za mapenzi na mapenzi kwa ujumla

 basi bwana mapenzi yakaendelea motomoto miezi ikapita ikafika kipindi yule mwanaume wake Neema kwa jina anaitwa Michael alitaka kumuoa neema na kuishi naye kama mkewe na kuanzisha familia akamueleza neema kwamba tokea nimekuwa na wewe sijapata kuona mwanamke mwengine ambaye nataka kuwa naye, umekuwa mwanga kwangu umeniletea faraja katika maisha yangu kutokana nahayo kwakuwa nakupenda sana nataka neema uwe mke wangu tuoane!!!!!

 Neema alifurahi akamkumbatia michael akambusu na kumwambia yupo tayari kuwa mke wake basi jioni ilipofika michael kama kawaida yake akamrudisha neema nyumbani neema alipofika tu nyumbani basi akaenda kumwambia ndugu yake astazia kwamba michael anataka kuja kuwaona wazazi wangu anioe

 basi michael na ndugu zake wakajipanga wakaenda kuwaona wazazi wa neema na kuanza process za ndoa

 process zikaanza neema akavalishwa pete ya uchumba, vikao vikaanza kama tunavyojua vikao huchukua miezi mitatu ndio shughuli basi vikao vikafanyika neema akapata watu wengi sana waliomchangia

  kumbe huku nyuma astazia alikuwa anawivu na roho kuumia kwanini ndugu yake amepata mwanaume wa kumuoa na ndoa wakati yeye yupoyupo tu na wote walikuwa umri mmoja

 basi kwakuwa alikuwa na number ya michael akaanza kumjaza maneno michael kwamba neema ni malaya yani anawanaume wengi amewapanga wengine wakumuhonga hela wengine sijui wakuhonga vitu pamoja na wewe yani usipoangalia utakufa kwa ukimwi maana yule hulka yake ni umalaya hawezi kuwa na mwanaume mmoja

 michael akamwambia sawa nimekusikia lakini unaushahidi kama kweli neema ni malaya??

 Astazia akamwambia wala usipate tabu nitakupa ushahidi, basi anastazia akamtafuta mkaka ambaye ni rafiki yake ila sio rafiki wa neema na wala neema hamjui akachonga naye dili na kumwambia atamlipa basi yule mwanaume anayeitwa peter akakubali

 Jamani hizi simu zetu za kisasa tunazipenda ila ndio chanzo cha matatizo basi anastazia akamrushia peter picha za neema nyingi tu hata ambazo huwa walikuwa wakipiga chumbani huku wamevaa kanga na nyengine neema amevaa tu chupi na sidiria zote akamtumia peter halafu yeye akazifuta zake kwenye simu yake

 siku hiyo akampigia michael kwamba wakutane ili ampe ushahidi huku michael moyoni yeye alikuwa haamini kama kweli neema anaweza kufanya hivyo lakini hakutaka kujiaminisha sana asije akaumia baadae

ILIKUWAJE BAADA YA MICHAEL KUFIKA SUBIRIA PART 2.....

0 comments:

Post a Comment