Tuesday, November 27, 2012

Majangaaa..

SIKU chache baada ya ndoa ya msanii wa filamu za Kibongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ kuvunjika, staa huyo amefunguka na kutaja chanzo cha kutengana na mumewe, Masoud Ally ‘Luqman’.

Akizungumza na paparazi wetu, Nora alisema kuwa, ndoa yake iliyodumu kwa mwaka mmoja ilitawaliwa na mateso ya hali juu tangu mapema lakini alivumilia kwa kuhofia kuonekana mkorofi ikizingatiwa kuwa ilikuwa ni ndoa yake ya pili.

 
“Miezi mitano baada ya kufunga ndoa hali ilianza kubadilika hasa baada ya kwenda kuishi kwa wakwe zangu Zanzibar, nilikuwa nikisimangwa waziwazi na kubaguliwa kwa kuambiwa wanawake wa Tanzania Bara hawafai,” alisema.
 
-“Pamoja na wakwe kunisimanga, walimtaka mtoto wao aoe mke wa pili wakidai kuwa ndiyo ndoa yetu itakuwa na amani na kunifanya niwe na heshima,” alisema.Nora alisema kuwa waliporudi Dar es Salaam, mumewe aliendelea kumtesa na kumfanya ashindwe kuvumilia.

“Kwa sasa nina amani sana kwani nilikuwa nimekata tamaa ya maisha kutokana na mateso niliyokuwa nikiyapata, afya yangu ilikuwa dhaifu, kila mtu akawa ananishangaa walionifahamu zamani walipokuwa wakiniangalia hawakunitambua kabisa,” alisema Nora.


No comments:

Post a Comment