Jamani ladies siku yetu ya kufundwa ndio hiyooo tarehe 7/12/2012 lipia nafasi yako sasa nipigie 0717 019320 kutakuwa hakuna malipo ya mlangoni mwisho wa kulipia ni tarehe 6/12/2012 watu wataanza kuingia ukumbini saa kumi na moja na kuendelea lakini kufundwa kutaanza saa moja usiku ili turuhusu watu kufika baada ya kutoka makazini ukiangalia foleni ni nyingi kwahiyo saa moja mafunzo yanaanza mpaka saa nne mpaka saa tano kwahiyo wenye kuomba visa muelewe wapenzi.
Chamuhimu kumbuka kuja na vest/singelndi yako nyeupe mkifika ukumbini wote mnatakiwa kuvaa vikoi na hizo singlend nyeupe kama unahisi wewe ni menene hupendezi kuvaa singlendi nyeupe vaa top nyeupe na kumbuka huku anayetaka kujaribu yaliyofundwa kama kukata kiuno unakaribishwa lakini kama hutaki basi mtabaki wasikilizaji tu.
Siku zimeisha uuwwiii sipati picha waulizieni waliokuja mwezi wa kumo huku ni moto narudia kama wewe unaaibu naomba uiache mlangoni na kama wewe ni mtoto huku usije utapofuka macho na masikio utuletee kesi.
Ninachokuahidi hutatoka kama ulivyoingia utajifunza mengi na mpenzio/mumeo atafurahi na ndoa/mapenzi yenu yatashamiri na MUNGU atazidi kuwabariki na najuwa mtanipigia simu kunishukuru kama waliokuja mwezi wa kumi walivyoona mabadiliko walinipigia na kushukuru sana hivyo ndio ninavyopenda hatufanyi biashara hapa tunafunzana ya muhimu yatakayotufanya siku UKIMWI uzidi kupungua maana wapenzi waume kwa wanawake hawatakuwa na sababu ya kutoka nje ya mahusiano yao.
Mwakani MUNGU akipenda tutafanya moja ambayo wanaume watakuwepo pia 26/4/2012 anzeni kuwataarifu mapema na kama kunawatu wanataka kuwa sponsors pia mnakaribishwa sana, tunataka kubadilisha jamii na kufanya ndoa kitu ambacho kila mwanamke na mwanaume ataithamini na kuipenda na kuitaka sio kuwaza nataka kuolewa nitoe nuksi HAPANA bali uutendee mema na haki mpango wa MUNGU.
Ahsanteni
No comments:
Post a Comment