Tuesday, August 21, 2012

Makubwa Haya..

Jamani baada ya kutuma ile post ya wizi mpya wa mjini haswa kwa wale chovyachoya mchuzi una ladha gani nimepata kihoja chengine hiki hapa;

Unaambiwa hapa mjini kila mtu anakula kivyake, watu wanatoka nyumbani wanaaga kwenda ofisini kutafuta riziki siku ya mwisho wa lete tonge mezani.

Unaambiwa kuna mkaka hapa mjini yani wanadai no mzuri hamna mchezo kijana kapanda hewani full kung'aa madini hapo nje anapark verossa yani wanaomjuwa unaambiwa akikutongoza kama wewe maharage ya mbea maji mara moja lazima uingie mkenge acha tu..

Sasa huyu yeye unaambiwa ananasa wamama wenye hela zao, wewe mwenyewe umejitokelezea full madini umependeza mwenyewe ukijiloga kuingia sehemu alipo na akagundua wewe mtu wa thamani lazima aje akufwate (uzuri wa huyu kaka yeye hakunaga umasikini anaangalia watu wenye hela zao maana mwenye hela bwana ukimtazama tu lazima uzione..hehe heiya) tajibeba sana mwaka huu

Basi kijana akishakugundua anakuja mwenyewe anamwaga sera zake shosti na yeye alivyokuwa wa maana ukijikita tu umekwisha shoga basi ndio katongozwa kaona mwanaume sindio huyu kwa nini asimkubali usiku wakaumalizia wote kumbe jamaa sijui anamadawa watu wameenda hotelini kama inavyokuwayule dada anasema akawa anakunywa wine mara akajisikia usingizi na kumuambia mpenzi walale mpaka baadaye kidogo ndio waendelee kuonyeshana ufundi alivyoamka kwani alimkuta kijana!!!!!chezea mji huu wewe

Kijana kaondoka kabeba hela zote za mwanamke, madhahabu yake aliyokuwa kayavaa usiku hule kamuachia nguo tu na pochi yenye kadi zake za benki (lol) unaambiwa mwanamke kuamka kugundua kashaingizwa mkenge ndio kutafuta mlango wa nyuma wa hoteli ndio kukimbia..

ONYO:

Jamani siku hizi hakunaga mapenzi utapeli mtupu..kuwa makini na unayemtaka na anayekutaka, magumegume kibao siku hizi..

No comments:

Post a Comment