nimeingia kwenye ndoa nikakuta mumewangu mwanzo alikuwa na mtoto ambaye sio mkubwa sana huyu mtoto alikuwa anakaa kwa bibi yake sasa mume wangu kaamua huyu mwanaye aje kuishi na sisi tatizo ni kwamba huyu mtoto jamani ananitega mwenzenu sijui kwavile anaona hapa kwa baba yake vituko haviishi tena vile vya kutia hasira mpaka wakati mwengine nataka kumbonda na kila niikimgombeza basi baba yake akirudi nyumbani anamwambia na mambo mengine ya uongo kunitia miye ubaya kwa mume wangu mpaka siku nyengine tunanuniana na mume wangu yani nyumba haina amani jamani nisaidieni nifanyaje?
sijui nikuite dada au mdogo wangu hayo tuyaache sio mahali pake hapa ila natakakukuuliza huyo mtoto mama yake yuu hai nauliza hivyo kwa sababu sio ajabu mama yake anamtuma aje akufanyie vitimbwi sasa dada lakufanya mwite mumeo pamoja na huyo binti aulizwe mbele yako km anatatizo nawewe na aseme mbele yako sijui huyo mtoto ana umri gani na mume wako aelewe kila kitu lakini isikute na wewe unamnyanyasa huyu mtoto maana wa mama wengine wanaroho mbaya na watoto wawenziye japo sina hakika nawewe pekee ndio unajijua lakini kabl;a ya yoote mtangulize mungu ndiye jibu la tatizo lako na hakuna linalomshinda halimradi tu usali kwa bidii na kumtegemea na kumwamini
ReplyDeletemimi nahisi unachotakiwa kufanya ni kuonyesha upendo kwa huyo mtoto. ukianza na tabia ya kusema huyu mtoto wa kambo basi na yeye pia atkutreat kaam mama wa kambo. ushasema huyo ni mtoto kwa hiyo ukimuonyesha upendo wa dhati na kumlea kama mwanao basi lazima atakuwa na heshima. na hiyo itakusaidia sana kwenye ndoa yako.
ReplyDeleteMimi nishalea watoto wa hivyo tena basi wala sio wa mume wangu ni wa ndugu zake. Yaani ile naolewa tu hata sijakaa vizuri na mume ndugu wakaanza kuleta watoto wao niwalee! Tena ndugu hao wengine wanaishi hapa hapa Dar na waume zao, yaani ilikuwa mashindano mpaka wanagombana. Sasa kivumbi watoto wajeuri kama nini kila siku visa na mikasa. Na huyo baba yao mdogo sijui mjomba sijui babu akirudi watakaa waseme umbea wee, mpaka unajiuliza hivi hawa ni watoto au mashetani. Wacha nikwambie kuna familia nyingine wanawatia watoto maneno makusudi ili nyumba ikushinde uondoke. Na wakishindwa kwa hilo watoto hao wanatumia mpaka kuleta mambo ya ushirikina ndani ya nyumba, nimeyashuhudia kwa macho mie mwenzenu. Kilichonisaidia ni elimu yangu na kazi yangu maana kama isingekuwa kazi na pato langu nahisi ningekuwa nalala na njaa, maana wakati mwingine wanakwambia leo tunapika hiki chakula, wao ndio wenye amri na maamuzi ndani ya nyumba!
ReplyDeleteMdogo wangu kwanini huyo mtoto asilelewe na mama yake mzazi? Kama amefariki hilo ni jambo lingine tafuta suluhu ya kumpeleka boarding ama sivyo hutakaa uone raha ya ndoa maana hata usemeje hutakaa uonekane mkweli kamwe maana damu ni nzito!
Mimi ni mume na nimekuwa na tatizo kama lako katika familia, ila naamini mke wangu aliathiriwa kisaikolojia na watu wake wa karibu. Kwamba huwezi kulea mtoto wa kambo. Believe mi kama unampenda mumeo na yeye anakupenda, basi hiyo ni ticket yako mzuri ya kuonyesha jinsi unavyoweza kuwa Waziri mkuu wa nyumba.
ReplyDeleteUshauri wangu ni huu. Huyo mtoto ni wa mume wako na ni damu ya mume wako. Tafadhali ondoa swala la mtoto wa kambo katika mawazo yako. Hili linaweza kukuathiri ki-saikolojia. matokeo yake inapunguza mapenzi kwa huyo mtoto.
Swala la pili muda wowote unatakiwa kujua kuwa kama ni mtoto basi wewe unatakiwa kutumia busara zaidi yake.Muonyeshe mapenzi na kuwa nae karibu utashinda
Kabla ya kuita kikao kati yako, yeye na baba, basi mueleze kuhusu tabia zake, pia mwambie kuwa hupendi kumueleza baba yake ila asipojirekebisha basi mmwambie hutakuwa na jinsi zaidi ya kumueleza