jamani kuna dada anauliza kama kwenye dini zetu kuna maandiko yeyote yanayomkataza mwanamke kuwa na mume mwenye umri mkubwa kuliko yeye.... kama unafaamu hebu mwelimishe huyu dada....
kwa mimi ninavyofahamu sijawahi kuona hayo maandiko na kwanza ukiniuliza mimi nitakwambia sio vibaya kuolewa na mwanaume mwenye umri mkubwa kwani mara nyingi hao huwa wanajuwa wanachokitaka katika ndoa na wake zao yani nikimaanisha wameshapitia mahusiano mengi na sasa ni wakati wa wao kutulia hawatakusumbua kama hawa vijana wanavyosumbua wake zao mara nyingi wake hujikuta wanalia kwasababu ya ndoa za na vijana waliolingana umri ama waliowapita umri chini ya miaka mitano...
ca muhimu ni juwa tu je wewe ni mwanamke wa kwanza anayekuoa ama alishawahi kuoa na kama alishawahi nini kilitokea mpaka akuoe tena? na pia juwa je anauwezo wa kukufikisha kimahaba kwasababu japo atakuwa mzuri kwako kwa kila kitu pia aweze kukufikisha kwasababu ili mapenzi na ndoa zidumu lazima mtimiziane haja zenu za sita kwa sita...
ukiachana na hayo hongera kwa kupata mpenzi na furahia masiha kwani huyo ndio Mungu aliyekuchagulia..
Kuwa na mume aliyekuzidi kidogo umri ni jambo jema kwa sababu atakuwa ametulia kimawazo na pia mtakuwa mnaheshimiana.
ReplyDeletetabia ya mtu haijarishi umri kama mtu anatabia nzuri na anajua nini maana ya kupenda haijarishi umri mkubwa wala mdogo. hao mafataki tutasema kuwa ndoa zao ziko salama au zimetulia?maana wanachukua hao vibinti na wake zao wamewaacha nyumbani au nao hawakufanya katika ujana wao?mume ni mume awe mdogo au mkubwa muhimu umpate mwenye tabia njema wapo vijana na wako makini na ndoa zao na wengine mumezidiwa umri ila munalia katika ndoa zenu kila siku. muombe mungu umpate mume mstaarabu na mwenye kujua nini maana ya ndoa.mi mume wangu nimemzidi miaka 2 lakini tuna miaka 5 katika ndoa yetu mapenzi yanaongezeka kila siku. namshukuru allah
ReplyDeletedadaangu hakuna dini inayomzuiya mwanamke kuolewa na mwanaume alie mpita umnri.
ReplyDelete