Wednesday, October 27, 2010

NIMEPATA MUME WA KUNIOA LAKINI......

Mama Mizizi, ninajambo kubwa sana ambalo sijui nitafanya nini nisipo pata mawazo kutoka humu kwenye hii blog kwanza kabisa mpo juu sana wote mnaoingia humu na michango yenu na topics zenu zinasaidia sana na kweli ni mambo ambayo hutokea kila mara kwenye hizi ndoa za kiafrica.
baada ya muda mrefu kutamani ndoa nashukuru Mungu amenipatia mchumba, lakini sasa mimi ikija mambo ya chumbani najuwa kabisa halalamiki hata kidogo labda ndio maana kanogewa akataka kumiliki kila kitu kabisa,ila tatizo ni kwamba ikija kwenye mambo ya kuwa mke yani kumuhudumia mume siwezi kabisa kwanza nikifikiria swala la kuamka na kumuandalia kwanzia maji ya kuoga na chai yani ndio nakufa kabisa.
na ukiachia hayo mimi kufua nguo zangu tu tabu sasa za mume itakuwaje? jamani naombeni sana msaada wenu kwa aliyepitia kama haya naomba unipe wazo la kufanya maana nahisi kuchanganyikiwa mpaka ndugu zangu wananiambia nisije kuolewa na kurudishwa kwetu kwasababu sijui kazi.
Leluu

3 comments:

  1. sasa hapo mdada kwanzanimechokaaa, unajua huo wote ni uvivu wala hakuna kingine unajua wewe umeathirika kisaikolojia tayari kichwani mwako ushajiwekea kuwa siwezi lakini haiko hivyo ma dia ndoa ni safari ndefu sio kulala tu kitandani ni zaidi ya hapo, na kumuhudumia mume ni kazi pia na hapo ndo penye ndoa, wewe unatakiwa ujitune mind yako kuwa sasa am going to do this and this na utashangaa pia na huo uvivu wote ulionao toa kabisa kichwani jizoeshe kuamka mapema ili ukiolewa iwe ni desturi,kufua ,kupika jamani mbona hizo ndo kazi za kike,sasa ma dia kama huwezi kuyafanya hayo ina maana ndoa hautaiweza na itakuwa ngumu kwako kwani hata ukiweka housigel ipo siku moja moja kazi unafanya mwenyewe au siku nyingine unapika mwenyewe,otherwise mmeo awe ni mtu poa yaani hamind sana kazi zote akifanya housgel,mi mume wangu hana tabu kama kupikiwa na housegirl hana shida as long mi nakuwa sipo ila nikiwepo anapenda zaidi nimpikie.
    Jitahidi tu ujitune mind yako ili uweze kwani vinginevyo ndoa hutaiweza shost tena yatakupata makubwa.

    ReplyDelete
  2. my dia hata cjui nianze wapi, bt kama mimi navoona kwanza lazima ujue mume wako ni wa aina gani, kuna waume wengine hawajali kabisa mke kumfanyia mambo yote hayo, mfanya kazi ndo anafanya, kumtengea mume chai na kumpikia cjui na nini ujue we hujaolewa kufanya hizo kazi bali ni toka enzi za mama zatu imekua ni hulka kwa wanawake kufanya hivyo, kwasababu mwanamke ndo alikua yeye mtunzaji nyumba na baba akenda kutafuta rizki kuleta nyumbani. kwa siku hizi wanawake na sisi tumekua wahangaikaji pia wa kuleta rizki majumbani kwetu, ndo maana tunawafanya kazi wa kutusaidia, kama hamna mfanyakazi utakuta wengine mume na mke wote wanasaidiana kwenye swala zima la kazi za nyumbani. wanawake bado tunaonekana sie ndo watunzaji wa nyumba yetu kwa hizi mila zetu za kafrika. lakini wewe unavosema hata kufua nguo zako mwenyewe ni kazi yaani hapo cjaelewa kama ni uvivu tu au ni malezi ulololelewa huwezi kazi, ctaki nikujudge hapo ntakua nakosea, ila kama ni uvivu tu besti inabidi uanze kuchangamka na kujifunza kazi za nyumbani, m.mke usafi nakumuhudumia mumeo kwa mapenzi yote. unaweza ukawekewa mfanya kazi bt mfanya kazi sio ndo achukue nafasi yako mpaka nguo za ndani za mumeo afue yeye, mambo mengine unafanya kwa mapenzi tu usione kama vile ni wajibu au nn, kama kumpikia mumeo chakula kizuri akafurahi, na we si una furahi pia, sisemi ni lazima na we umeolewa kumuhudumia mume ni mapenzi tu yanatufanya tuwe tunaandalia waume zetu. wanaume walio wengi wanapenda mwanamke mwenye kumtunza ndo maana wakiona hamna matunzo kwa wake zao haooo wanaenda nje, lakini haina maana hata ukimfanyia yoe hayo hataenda kwa wanawake wengine, maana wanaume hawa hawana shukurani, ndo hapo inakuja mpende akupendae asiekupenda achana nae.
    tumtum

    ReplyDelete
  3. OVYOOOOOOO,SASA SIFA?????

    ReplyDelete