Thursday, October 21, 2010

KUMFUNDISHA MTOTO KUPIGA MSWAKI...



wazazi mliotangulia hebu nisaidieni nataka kujuwa jinsi mtoto anavyofundishwa kupiga mswaki maana naona wakwangu kila ninachomwambia afanye anafanya kinyume chake...
nikimpa maji asukutue mdomo nikimwambia tema anameza, nikijitahidi kumpigisha mswaki na kumuonyesha kutema dawa yeye anameza, uuiiii
hii ni kawaida ama nahitaji kumfundisha kwa njia nyengine???

5 comments:

  1. kwanza nenda naye sehemu mnayopigia mswaki ili akuone unavyo fanya. Kisha mwanzishe bila kutumia dawa (kuna dawa za watoto ambazo sio kali sana, kama unaweza mnunulia akkanzia hizo). Kila kitu kinataka uvumilivu, pole pole ataweza tuu.
    (NB: Hivi ulishawahi kujiuliza wewe mwenyewe ulijuaje kupiga mswaki?, neda naye pole pole...)

    ReplyDelete
  2. Umenifurahisha sana maana wa kwangu pia humeza,siku nyingine hataki kupiga mswaki yaani ufanye kazi kubembeleza

    ReplyDelete
  3. Na mimi wa kwangu siku nyingine anapiga vizuri siku nyingine mpaka umtishie monster!

    ReplyDelete
  4. wangu pia anameza jamani

    ReplyDelete
  5. mwanzo mgumu kwa kweli. watoto wengi wanameza dawa au maji wanapoanza kupiga mswaki. Uvumilivu ni nmuhimu sana. unachotakiwa ni kumnunulia mswaki laini, dawa za meno za wototo(wengi wanapenda flavour zake) na pia usimlazimishe sana manake anaweza kuchukia kusafisha meno kabisa. Angalizo kubwa hapa ni kuhakikisha maji ya kusukutulia yamechemshwa ili hata akimeza yasiwe na madhara si unajua maji yetu ya bomba?

    ReplyDelete