Tuesday, July 20, 2010

WANAGOMBANIA NDIZI WAKATI MGOMBA SI WAO...

mara nyengine sisi wanawake tunapenda kweli kujiabisha jamani, kuna wadada wawili wanamgombania mume wa mtu yani huyo baba ni mburundi anayeishi hapa mjini na familia yake nakama pesa kweli anazo nahisi ndio maana hawa wasichana kutwa wanagombana..
huyu mwanamke mmoja wa nje siku yupo ndani na yule baba mwanamke mwengine akatuma msg ya kimapenzi kwenye simu ya huyo mburundi wakati huyo baba anaoga yule dada akachukuwa simu na kukuta hile msg na kuchukuwa namba wakaanza kubaruzana sasa nje..
yani ugomvi mkubwa mpaka kutishiana kulogana na kuharibiana maisha, huyu msichana mmoja ni rafiki yangu mzuri tu, sasa kila mara wanapogombana najitahidi kumwambia kwanini mpaka wapigane kwa mwanaume ambaye sio hata mumewe mwenye mume katulia nyumbani kutwa hawa mahawara wanataka kutoana roho..

KWA WANAWAKE HAO

hivi wewe mwanamke kweli unagombana na mwanamke mwenzako kwa mwanaume asiyekuhusu kisa hela? kwasababu hebu fikiria mpaka mgombane huyo mwanaume angekuwa anataka kuwa na mwanamke mmoja wa nje huyo wa pili alikujaje? ukiona hivyo ujuwe anataka pia kuwa naye kwahiyo kwanini mgombane..
unajuwa kama msichana ambaye hujaolewa pale mume wa mtu anapokuta unajiona wewe ndio wewe kwamba wewe ni mzuri sana ndio maana ameo na bado anataka kuwa na wewe hivyo ndivyo tunavyo jidanganya hata mimi nilipitia huko, kitu ambacho sio kweli wanaume wengi hupenda tu kuwa na mwanamke wa pembeni sio kwamba hawawapendi wake zao ila starehe tu na uzinzi umewajaa kwani kama wangekuwa wanataka sana hao wanawake wa nje si wangewaacha wake zao ili wawe na hao wa nje...
wanawake tusiwe wapumbavu akikuchoka wewe, ataenda kwa mwengine na bado atamkimbilia mke wake nyumbani, kama unadhani huyo mume wa mtu anakupenda kwa dhati hebu jaribu kumshawishi aachane na mkewe uone kama atamuacha...
wakati wa wewe kuolewa ukifika amini utakuta mumeo pia anatoka nje yani hilo ni jambo la kawaida sio la kushangaza sasa kwa nyie mnaotaka kutoana roho acheni upumbavu kama mpo kwa huyo baba kwasababu ya hela chumeni hela muendelee na maisha..maana mtaendelea na maisha yenu na yeye na yake na mkewe mgomba unamwenyewe tena mama wa kiburundi ndio kashaingia hata kwa chopeo hatoki yule wewe kula tu kimya kimya.

1 comment:

  1. na tujifunze kuacha ubinafsi unajua mtu ameoa nawe unatongozwa unakubali...si kwamba hapendi mke wake ni tamaa nawewe usipokemea ndo utashangaa atakuchezea na kukuacha..tunawaona wengi wanshoboka na pesa za wanaume wa watu..wananunuliwa magari, wanapewa funguo kadi wanasikia redioni,wanapangishaiwa partment na kila kitu ujuacho but ukiisha thamani anatafuta mwingine mpya, na gari yake anakunyang'anya kwa kukutafutia ababu ndogo tu...utaJUTA..mana unaachwa mweupe back to square one. tusijidanganye kina dada mume wa mtu sumu..tujifunze kufight for life na sio ku fight against one another tena kugombea mwanaume?! khaaaaaa......zilipendwa

    ReplyDelete