wasichana wa kazi ni watu muhimu sana katika maisha yetu haswa kwa wanaoishi na familia pamoja na watoto, kwani hawa ndio wanaotusaidia kuwatunza hawa watoto na nyumba pindi ambapo hatupo nyumbani, lakini je unajuwa jinsi ambavyo unampata huyo house girl wako na je wakati unatafuta house girl wakukaa na watoto wako na nyumba yako unajuwa anatokea sehemu gani na familia yake ni watu wa aina gani na kabila?
limemkuta rafiki yangu mmoja, yeye anaishi na mumewe, mdogo wake na mtoto wao mmoja pamoja na mfanyakazi (housegirl) huyu mfanyakazi kama ni kazi kwa kweli anajitahidi sana ni msafi, na kazi zake anaweza kweli kuzifanya vizuri na kwa muda unaotakiwa huwa amemaliza zote pamoja na kuweza kumtunza vizuri mtoto.
lakini ubaya wa yule msichana wa kazi hataki kabisa kufokewa, yani yeye ukimfokea tu anatishia kuondoka ama kufanya kitu kibaya hapo nyumbani, sasa siku moja yule dada rafiki yangu akamuuliza yule msichana kwa nini wewe ukifokewa unakuwa unakasirika mpaka kunitishia humu ndani inamaan heshima na boss wako huna sasa hapo tu nakufokea kwa sababu ya mambo yako madogomadogo unadhani siku ukifanya kosa kubwa nitashindwa kukufokea kisa naogopa utanidhuru?
yule msichana wa kazi akamwambia "dada unadhani nitakudhuru nitakachokifanya nitakuomba hela yangu ya mwezi unipe halafu ukiwa umeenda kazini nitambeba mtoto niondoke naye halafu wewe utanifwata songea kwa miguu" looooooooo jamani haya ni maneno yakumwambia mtu mwenye mtoto, yule rafiki yangu presha juu hivi anataka kumfukuza lakini anawasiwasi asije akarudi yeye akiwa kazini.
tuwe makini jamani na hawa wasichana wa kazi..
No comments:
Post a Comment